Hivi yule 'Babu wa Loliondo' bado anatibia?

Hivi yule 'Babu wa Loliondo' bado anatibia?

Ulimakafu

JF-Expert Member
Joined
Mar 18, 2011
Posts
31,248
Reaction score
13,244
Vile vikombe vilivyokuwa vinaibuka kila uchao siku hizi havisikiki tena,Si kwa babu,Tabora,Mbeya wala wapi sijui au ndo tunapisha bunge kwanza ndo viendelee?Au huduma imesitishwa?Mlioko kwenye maeneo ya tukio/mwenye habari tujuzeni.
 
maandamano, richmond na dowans vilipoondoka singo za vikombe nazo zikaondoka!! Kuna singo mpya inakuja hii ya shimbonyi... namaanisha simbioni pindi pale makali ya umeme yatakapokolea katikati ya mwezi ujao na mwanzoni mwa mwezi wa nane!! Machungu yatakapoongezeka sasa watazuka mabinamu na mashangazi watakaokuwa wakutoa majagi na magudulia ya dawa!!!
 
we hujui kwamba idadi ya watu waliotakiwa kupigwa chapa imeshakaribia kufikia? sa hv wanaoenda ni wachache na mda si mrefu huduma itasitishwa.
 
Vile vikombe vilivyokuwa vinaibuka kila uchao siku hizi havisikiki tena,Si kwa babu,Tabora,Mbeya wala wapi sijui au ndo tunapisha bunge kwanza ndo viendelee?Au huduma imesitishwa?Mlioko kwenye maeneo ya tukio/mwenye habari tujuzeni.
Mi nilijua kipindi hiki cha heka heka ndio watu fulani watachukulia opportunity kum-promote babu ili kutufanya tuongee vya vikombe zaidi na tusifatilie yanayo tokea bungeni ila naona kimyaaaaa... tungoje tuone
 
Raia walikuwa hawasikii lolote juu ya tiba ya babu...sasa hivi walioenda mmoja mmoja anarudia dawa zake.
Watu wangu wanaangamia kwa kukosa maarifa...Neno la Bwana lasema.
 
Loliondo Kikombe bado kipo na kuna magari si chini ya 200 kila siku ila mengi ni kutoka Nchi jirani hasa kenya, Uganda, Rwanda na nimeona watu toka hata Zambia. Nilikuwa huko Ijumaa.
 
Kikombe halisi kipo kwa babu Loliondo. Mimi ni shuhuda,nliku na BP. Baada ya kunywa, sasa hivi miezi minne niko fit.

Asante kwa ushuhuda,vipi 'utendaji wako' nao uko kwenye mstari?
 
Babu wa Samunge bado anapiga kazi bila kupumzika!
Shida Watu wanataka waone maandishi na Picha kwenye magazeti ndio wajue kinachoendelea Samunge!
Tuulizeni tunaojihusisha na mambo ya huko tuwajuze yanayojiri!
Kwa report yenu ni kwamba SASA HIVI NDIO WATU WENYE PESA YAO WANAENDA KWA BABU, na wanahudumiwa bila bugza!
Foleni bado zipo, japo anamanage kuhudumia wote!
Watu wasikurupuke kuongea wasichokijua!
JWTZ ndio kwanza wanaweka kituo chao hapo ili kuhakikisha usalama, na bado mambumbumbu wengine wanategemea huduma zimepungua!...Shiiit!
 
Babu wa Samunge bado anapiga kazi bila kupumzika!Shida Watu wanataka waone maandishi na Picha kwenye magazeti ndio wajue kinachoendeleaJWTZ ndio kwanza wanaweka kituo chao hapo ili kuhakikisha usalama, na bado mambumbumbu wengine wanategemea huduma zimepungua!...Shiiit!
PJ umesema yote, waambie hao waropokaji
 
I never trusted Babu.... aiseee nilikua nikangalia eye contact za Babu akiwa anaongea unajua kabisa anadanganya... May God reward him accordingly
 
Sina tatizo na babu kikombe chake, mimi nina tatizo na mungu wa babu! Mwanzo alituletea DECI akatula! Sasa ametuletea KIKOMBE katupata! What next?
 
Kuna mama mmoja jirani yangu alienda kwa Babu, alikuwa na Presha saizi anasema ndio anaumwa sana ndugu zake wanapanga kumpeleka India, Babu anawandanganya sana watu
 
wanaJF samahanini kama nitakuwa nawaboa na mada ya huyu mzee aliyejinyakulia umaarufu miezi michache iliyopita namaanisha Babu Mwasapile wa Loliondo.

Najua kutibiwa au kutafuta tiba ni jambo la binafsi lakini kwa kipindi kile sio rahisi kuamini kuwa lile jambo lilikuwa na kibinafsi make hata serikali ilimsapoti sana kufikia hata kutengeneza barabara ya kuelekea kwake.

Sasa swali langu ni kwamba najua kuna baadhi humu JF mlienda huko Loliondo au mna ndugu zenu walikwenda ,Je? dawa ya huyu 'babu' ilikuwa effective'?. Na kwa wale mliopo maeneo hayo ya Loiliondo hivi ile misafara bado inabamba?

Au huu mgawo wa umeme umemuathiri na yeye?
 
Anatoa dozi kama kawa. Nenda biafra kuna magari yanatangaza ratiba ya ya Loliondo, nenda ukapate latest info
 
Babu kama kawa anatoa dozi kikombe kimoja jero wahi sasa kabla foleni haijarudi tena kuwa kubwa.
 
Na Ashe Hassan


Mtoto Subira Ally (12), Mkazi wa Kijiji cha Malema, Kata ya Maratani, wilayani Nanyumbu, mkoani Mtwara ameonekana kumpindua Babu wa Loliondo, Mchungaji Ambilikile Masapile (pichani) kwa kupata wateja wengi ambao wanakwenda kutibiwa.

Kupinduliwa kwa Babu kumetafsiriwa na watu baada ya kuonekana sasa nyumbani kwake Kijiji cha Samunge hakipati wageni wengi kama ilivyo Kijiji cha Malema anakokaa Subira ambako wageni kutoka mikoa mbalimbali na nchi jirani hufurika kila kukicha.

Akizungumza na mwandishi wa habari hii hivi karibuni, mtoto Subira alisema kuwa siku moja , Aprili mwaka huu akiwa amelala alioteshwa ndoto iliyokuwa ikimuelekeza kuwa anatakiwa atoe tiba kwa njia ya kikombe kwa kutumia mzizi wa mti uitwao Mkong'oto unaopatikana hapo nyumbani kwao, hivyo kumjulisha mama yake mkubwa anayeishi naye.

"Niliambiwa kuwa dawa hiyo itakuwa inatibu Ukimwi, kisukari, kuponya vipofu, viziwi, na wote ambao miili yao itakuwa imekufa ganzi au kupooza," alisema Subira.

Aliongeza kuwa dawa hiyo ya kikombe alioteshwa kuwa iwe ikinunuliwa kwa gharama ya shilingi 500. Alipoulizwa ni watu wangapi ambao amewatibu tangu alipoanza kazi hiyo alisema ni wengi sana.

"Wagonjwa ni wengi sana ambao wamepata kikombe na wanaendelea kufika hapa nyumbani," alisema huku akiwa na mama yake mkubwa aliyefahamika kwa jina moja la Binti Ismail.

WAGENI TOKA NJE YA NCHI

Subira alisema licha ya kutibu wananchi wa Tanzania, amekuwa akipokea wageni wengine kutoka nje ya nchi kama vile Msumbiji na Malawi.

Aliongeza kuwa licha ya wagonjwa wengi kutoka Tanzania bara, amepokea wengine kutoka Visiwani Zanzibar na anakumbuka mmoja alikuwa na matatizo ya miguu ambayo ilikuwa imekufa ganzi kwa miaka mitano. "Sasa mgonjwa huyo wa Zanzibar ganzi imekwisha na anatembea vizuri, amemshukuru sana Mungu." Mama mkubwa wa binti huyo, aliyefahamika kwa jina la Binti Ismaili alithibitisha mwanaye kuoteshwa na kutoa tiba hiyo.

MASHUHUDA

Naye mama mmoja aliyejitambulisha kwa jina moja tu la Sharifa mkazi wa Tandika Mikoroshini jijini Dar es Salaam aliyezungumza na mwandishi wetu hivi karibuni alisema kuwa, alikuwa muathirika wa ugonjwa wa Ukimwi lakini baada ya kutumia dawa ya mtoto huyo na kwenda kupima ameonekana hana virusi vya maradhi hayo.

"Baada ya kutumia dawa ya Mkong'oto nimepona,nilikwenda kupima katika Hospitali ya Maratani mkoani Mtwara na kuthibitishiwa na daktari aliyenipima aitwae Dk.Namihambi kuwa sina virusi. Nangoja kupima mara ya pili kwa uhakika zaidi," alisema.

Aidha, baba mmoja ambaye aliomba jina lake kuhifadhiwa alisema kuwa alikuwa na ugonjwa wa Ukimwi lakini sasa hana baada ya kupimwa katika Hospitali ya Mkomaindo, Masasi.

WAZIRI WA AFYA ALICHOSEMA

Mara baada ya Babu Masapile kutangaza kuoteshwa kutoa tiba ya magonjwa sugu, watu wengi wameibuka kutoa tiba hiyo na wananchi kufurika kupata kikombe.

Hata hivyo, wiki iliyopita gazeti hili lilimkariri Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Dk. Hadji Mponda akisema kuwa katika tafiti za kitaalamu dawa za mitishamba hazijathibitishwa kutibu Ukimwi.

Kauli hiyo ilitolewa na waziri huyo wakati anazindua Kituo cha Matibabu ya Wagonjwa wa Ukimwi na Mafunzo katika Hospitali ya Mnazi Mmoja, jijini Dar es Salaam hivi karibuni.

Dk. Mponda alisema wagonjwa wa Ukimwi wanatakiwa kutumia dawa za kurefusha maisha (ARV) na akawataka waende kwenye vituo vya afya kupewa."Wagonjwa wanaokwenda kupata tiba asili waache kwa kuwa bado zinafanyiwa utafiti," alisisitiza Waziri Mponda.
 
Back
Top Bottom