Hivyo ndivyo vijana wa kazi wa Kitanzania wanavyoturudisha nyuma na kututia hasara kubwa

Hivyo ndivyo vijana wa kazi wa Kitanzania wanavyoturudisha nyuma na kututia hasara kubwa

Nikifa MkeWangu Asiolewe

JF-Expert Member
Joined
Feb 26, 2024
Posts
6,944
Reaction score
14,351
Wana jukwaa heri nyingi kwenu nyote.

Tuko hapa jukwaani kutaniana, kukosoana, Kushauriana, kuelekezana kuhabarishana na mengine mengi.

Mara ya kwanza kujiunga hapa jf ilikuwa 2012 yote Kwa yote nilipendezwa na kuvutiwa na hayo machache niliyotaja hapo juu.

Miezi michache iliyopita niliandika Uzi uliokuwa unasomeka...

NIMELIMA NYANYA HEKA MOJA NA KUPATA MILIONI 15.

Kama mjuavyo hapa jukwaani wapo waliokubali na kuvutiwa na kutaka kujifunza zaidi wengine walisema haiwezekeni na wengine wakaenda mbali zaidi Kwa kusema na danganya. Yamkini baada ya kurudia hesabu vizuri na Kwa ufasihi niligundua nilipata kiasi Cha milioni 17 na 21 Elfu. Na sio m15 pekee kama mwanzo. Hii ni baada ya mdau mmoja kunihoji maswali ya kina ilibidi nirudi nikaanze upya.

Kwa vile ni kazi ninayo ielewa na Mimi ndo muhusika sikujali.

KILICHONILETA HAPA KWENU NI MASITIKIKO MAKUBWA SANA KWA VIJANA, WATANZANIA WENZANGU.

Iko Hivi baada ya kulima na kupata kiasi kile Cha pesa nilisafiri kutoka eneo nilikuwa Nimelima nikaenda kukodisha heka4 lengo nilime heka2 cabbage na heka2 mahindi ya kumwagilia(ya kiangazi)

Kama kawaida niliondoka na kwenda kukodi hizo heka 4 na Kila Hela nilikodi Kwa 80k maana zilikuwa mwambao wa Ziwa Victoria.

Tukaanza maandalizi mbegu tukasia ikaota vyema. Kazi ilianza Kwa nguvu sana.
IMG_20240716_073451_497.jpg

Ikumbukwe niliondoka na vijana wangu wa kazi wote4.

Kati Ya hao wa4 mmoja ndo alikuwa supervisor wao na istoshe alikuwa ni ndgu (Binamu) mtoto wa shangazi.

Jamaa huyu alikuwa na familia yake yenye watoto5 Jumla yeye na mkewe watu 7

Mwanzo nilikuwa namlipa kama wafanyakazi wengine japo yeye ndo alikuwa na uzoefu zaidi ya hao hivyo nilikuwa namlipa zaidi.

Baada ya kulima nae sehemu Moja kabla hatujalima hii niliyoisemea hapa kuwa nilipa m15. Nilikuwa Nimelima nae sehemu nyingine nyanya pia japo heka haikufika.

Nilikaa naye nikamwambia ndg yangu nimeona jitihada zako Sasa nahitaji tuwe tunagawana sawa yaani usimamie shamba kama lako tutakachokuwa tunapata tunatoa gharama zangu zote Kisha Hela iliyobaki tunagawana nusu kwa ½.

Jamaa yangu alilipokea Kwa furaha sana hili wazo langu ndipo tukaanza kulima na hatimae kupata hiyo 15m.

Baada ya kufika kule shamba nilikodi vyumba 2 Ili yeye awe huru hata mke wake akija basi wawe pamoja au hata Mimi nikienda (Boss wao) nipate sehemu ya kulala.

Nilinunua mahitaji yote yanahitajika na kama haitoshi nikanunua na mtungi wa gesi ule mdogo Ili kuwapa urahisi wa kuwahi kupita.

Hawa jamaa wote nilikuwa rafiki Yao mzuri sana. Niliwanunulia na pikipiki Sanlg Ili iwape urahisi wa kubeba vitu vya shamba kama water pump, pipe nk.

Kwa kifupi tu Ile shamba ya cabbage na mahindi Ili nigharimu kiasi Cha zaidi ya shilingi 4 milioni hapo najumuisha Kila kitu yaani vifaa vya umwagiliaji magodoro nk.

Binafisi Mimi nafanya kazi sehemu nimeajiriwa hivyo Huwa na mapumziko mafupi tu na nilijitajidi kuwa naenda na hata kwenye upandaji nilihusika Kwa 95% maana nilitoka pamebaki kidogo nikarudi kazini.

Nikiwa kazini jamaa(supervisor) akanipigia simu akinipa ushauri akisema.

Tangu tumalize kupanda na kama unavyojua Kwa Sasa kumwagilia ni mara Moja tu Kwa wiki yaani tukimwagilia jtano Hadi jtano. Hivyo Hawa madogo wanashinda wamelala ni kula na kwenda kutembea tu kusaka wapi Kuna disco vumbi na mabechiano(Sijui kiswahili fasaha Cha neno hili nitaelezea Kwa comment).

Jamaa akasema hivyo nilikuwa nashauri warudi kwao Kwa Sasa Mimi nitakuwa natumia vibarua wa kulipa Kwa masaa ambapo Kwa siku nikileta vijana watatu kumwagilia kuanzia saa9 Alasiri Hadi saa 1 tayari tumemaliza nawalipa Kila mmoja 2000 na hawali.

Kusema ukweli niliona wazo lake ni jema na nililipokea bila kusita.

Niliwapigia simu wale madogo nikawaambia na wao kweli walikili kazi hamna ndio maana wanaenda kutembea tu.

Nikawaambia kwa sasa nasitisha kidogo mkataba wao Hadi pale itakapohitajika ila Hela zao za mwezi huu ambao haujaisha nawalipa zote.

Hawakukataa waliokubali kesho yake nikafanya malipo kwa njia ya simu nikiwapa na bonus ya nauli na pesa ya kula njiani Nje na mkataba.

Kumbe lengo la jamaa lilikuwa abaki huru mazee. Kipindi akiwa nao walikuwa wakiniambia nitume Hela ya nyama Kwa watu wa 4 nilikuwa natuma kg 1 ya nyama kwa sababu dagaa samaki kama kambale walikuwa wanapatikana hata Kwa kutega na ndoano tu walikuwa wanapata.

Maharage dagaa tulikuwa tuna nunua Kwa mwezi.

Jamaa nilikuwa nikituma hiyo Hela mfano nikituma 15k-20k hii ni pamoja na vocha zao yeye nyama ananunua nusu kg tu asee na kuhusu vocha atawanunulia za jero tu.

Waliwahi kuniambia ila alijetete kuwa Hela nyingine aliongezea kwenye matengenezo ya pikipiki kitu ambacho haikuwa kweli.

Huyu jamaa pikipiki alikuwa anakodisha kwa siku analipwa 10k ikiharibika naambiwa mimi kutoa Hela ya matengenezo na nafanya hivyo.

Jamaa Ile water pump alikuwa anakodisha vilevile analipwa 20k Kwa siku alikuwa anakoshia wakulima wa tikitiki na mpunga wa kiangazi na hata wa mahindi pia.

Katika kukodisha akakodisha kwa jamaa mwingine ambae anatuhuma za uzinzi huyu jamaa alikodi Kwa siku 2 maana kazi haikuisha ikabidi pipe waziache hukohuko shambani kuepusha kazi ya kubeba na kuja kunyoosha pipe tena.

Usiku ule ule wakaingia wahuni wakakata Ile pipe yote vipisi vipisi ikabaki mita 100 nyingine ambayo haikuguswa.

Hii walimfanyia Moja ya watu anaozini na wake zao (Uzinzi mbaya). Pamoja na hayo yote na mengine yote jamaa hakuniambia kabisa.

Kila siku tunawasiliana anasema mazao yapo vizuri kabisa. Nikiwa kazini nikapigiwa simu na mwenye shamba akisema.

Boss mbona shamba umeikimbia? Nini shida mazao yameanza kukauka kabisa mahindi kidogo naona yanaendelea Endelea umekwama wapi boss?

Nikashangaa nikamwambia acha utani boss wangu siwezi shindwa shamba kama Ile asee. Akarudia sikutanii na huwa sina utani nawewe ukweli kwamba wafanyakazi wako hatuwaoni wiki3 hii sijaona mtu yeyote jana nimepita hapo walipokuwa wanaishi nimeambiwa wamesafiri.

Nilipigwa na butwaa sana muda huo nikamwambia tu ngoja nikawa nimemkatia simu. Ikumbukwe jamaa tumetoka kuongea nae kama dk9 tu zilizo pita ananiambia nitume Hela ya mafuta na vibarua kesho amwagilie!

Nikampigia akawa kwenye kelele akaniambia ngoja atanipigia. Muda huo nikampigia mwenyeji wetu aliyetuunganisha kupata shamba.

Hapo kulikuwa na kijana ambaye alikuwa anahusika kuja kufanya kazi Kwa malipo ya kutwa. Huyu ndo aliyeniambia haya yote kuhusu pikipiki na water pump kukodishwa nk.

Kichwa kiliwaka moto sana hasira ikapanda nikanywa maji kama lita1 Hivi yaani kopo la maji ya Kilimanjaro lote.

Dogo yule akanihakikishia kuwa kwenye kabeji hatuwezi ambulia kitu chochote zimeliwa na panzi na zingine zimekauka kabisa.
IMG_20240715_184633_385.jpg

Kwa sasa ni heri Uajiri watu kutoka Burundi kama Sheria ya Nchi itaruhusu kufanya hivyo ni Bora sana.

Hawa jamaa (warundi) nimefanya nao kazi sana kwenye kazi zangu. Wanajituma hawana kinyongo, hawana maneno Wala kubagua chakula wao kikubwa maharege yawepo tu basi hata kama mafuta kupikia usinunue ni vitu vya ziada tu kikubwa chumvi na maharage yawepo mambo ya mafuta vitunguu nk hawana habari navyo sana na hata ukiwauliza mahitaji ni ngumu sana kukutajia na mfuta ya kupikia na vitunguu. Utasikia mahindi yameisha maharage, dagaa zipo kidogo. Simple sana.

Jamaa wanashinda kazini na wanaweza wakawa na ratiba ya kula jioni tu. Hii wanajipangia wao wanakwambia kabisa sisi kupika mchana tunachelewa kuanza kazi.

Nasema haya nimewahi fanya nao kazi Kwa miaka4 tofauti tofauti.

Shida Sasa Hivi ukimatwa unao bila vibali asee ni kosa kubwa sana lakini watu na nusu Hawa hawana wivu kabisa na ukitaka uwafaidi wabatize majina hata yakisukuma ama hata kichaga sawa tu na kamwe usiwaite warundi umekosea sana Waite waha.

Watakupenda mno mwaka utaisha hakuna hata mmoja atakuambia arudi kwao akasalimie ni hakuna sana sana wakianza kuzoeana na wenzao walio tangulia huku na kuambukizwa tabia za kibongo Wana warubuni na kwenda nao mjini.

Nilianza kujiuliza maswali kama haya jamaa kumbe ukisikia boss kapiga mfanyakazi risasi usihukumu na kumuona Mnyama pengine huyu mfanyakazi ndo Mnyama zaidi ya boss wake.

Imagine inawezekana vipi uache shamba la mtu bila taarifa hajakukosea Wala hujamkosea unaamua kutelekeza shamba huku ukimpa matumaini hewa je, ukiadhibiwa utasema umeonewa?

Millioni 4 ni pesa ndogo kwenu ninyi madone lakni kwangu Mimi hata iwe laki1 tu huwezi kuifanyia ujinga wa hivyo asee.

Huwezi amini hapa kila kitu kiliharibika kabisa maana Kila kitu huenda na malengo nilikuwa na malengo lakini baada ya hapo malengo yote yakazima kama mshumaa kuanza tena hadi mwakani.
IMG_20240715_184522_913.jpg

Nilikuwa na makadirio ya kutoa angalau milioni22 Kwa heka hizo mbili maana Kila heka ya cabbage iliingia mashina 8000+ Kwa mahindi sikuhesabu nilipanga nihesabu yakiota na kukua vizuri.

Video hii hapa.

Kamese usimuamini mfanyakazi hata siku moja, wana unaa sana;mwaka 2018 nililima tiki tiki maji maji kigamboni sehemu inaitwa tundwi songani nikaweka vijana wa 3 mmoja mzaramo wengine wawili wasukuma;bwana wale wasukuma wanapiga kazi ila mmoja nikiboko akisha kula jani ni kazi,mimi nikawa naenda nakurudi maana nilikuwa na gari,mara nyingine nakaa hata wiki.

Wakati wa kupanda nilimteua huyo mzaramo asimamie;bwana we nilinunua kopo Za mbegu gramu 500 mbili kwa heka mbili huwa zinatosha lakini cha ajabu ziliisha na shamba alikuisha nikapigiwa simu mbegu zimeisha,kesho yake nikafuata mbegu kariakoo Za kumalizia,kama 250gm,bado hazikutosha ikabidi niulize mbona siwaelewi wakati mbegu ni hesabu mnafanya nini? Wakasema hamna kitu,mbegu zilipokuja kuota subanallah shimo moja miche 50,20,nikawaita yule mzaramo hakuwepo,ndio wakaniambia alikuwa anamwaga yeye,aise nilimtafuta,na nilimpa na kisimu,akajichanganya akaonekana,aise nilimtandika karate sio poaa,na nilisema Niki kukuita road nakupitishia tairi,alikuwa anions gari yangu Ana kila Nyoya,final napiga Hesabu 10M+zimepotea nikaja kuvuna hata 5M sikupata tangu hapo simuamini mfanyakazi
 
Shida ni kwamba wao hujiona wamekomoa na wanajiona ni mabingwa bila kujari maisha yao yatakuwaje kama wataharibu hapo. muathirika mkubwalazima awe yeye
 
..Pole sana ndugu, mimi nilinunua miche ya Minazi mingi ya kutosha shamba la heka 6, msimamizi wangu ndiyo alitafuta vijana wa kusaidia kuchimba mashimo ya kupanda, ikapita miezi kama 3 hivi, nikawa nakagua mistali nikakuta kuna mistali imeng'olewa!, nilipochunguza kimya kimya kupitia watu wengine nikaelezwa yule kijana wangu ndiyo aliyeiba ile miche..
 
Hatari sana na hapo aliuza kwa bei ya nyanya tu
 
Kamese usimuamini mfanyakazi hata siku moja, wana unaa sana;mwaka 2018 nililima tiki tiki maji maji kigamboni sehemu inaitwa tundwi songani nikaweka vijana wa 3 mmoja mzaramo wengine wawili wasukuma;bwana wale wasukuma wanapiga kazi ila mmoja nikiboko akisha kula jani ni kazi,mimi nikawa naenda nakurudi maana nilikuwa na gari,mara nyingine nakaa hata wiki.

Wakati wa kupanda nilimteua huyo mzaramo asimamie;bwana we nilinunua kopo Za mbegu gramu 500 mbili kwa heka mbili huwa zinatosha lakini cha ajabu ziliisha na shamba alikuisha nikapigiwa simu mbegu zimeisha,kesho yake nikafuata mbegu kariakoo Za kumalizia,kama 250gm,bado hazikutosha ikabidi niulize mbona siwaelewi wakati mbegu ni hesabu mnafanya nini? Wakasema hamna kitu,mbegu zilipokuja kuota subanallah shimo moja miche 50,20,nikawaita yule mzaramo hakuwepo,ndio wakaniambia alikuwa anamwaga yeye,aise nilimtafuta,na nilimpa na kisimu,akajichanganya akaonekana,aise nilimtandika karate sio poaa,na nilisema Niki kukuita road nakupitishia tairi,alikuwa anions gari yangu Ana kila Nyoya,final napiga Hesabu 10M+zimepotea nikaja kuvuna hata 5M sikupata tangu hapo simuamini mfanyakazi
GT mrangi njoo faster huku usome kuhusu matikiti.
 
Hakika mkuu kumbe ukatili husababishwa sisi wenyewe
Mjerumani alikuwa na kauli mbiu nigger bila mboko hasikii na hatasonga. Na kweli mjerumani alikuwa anatembeza bakora balaa. Hata mama anatakiwa atembeze tu fimbo kwasababu kuna watu wamemzoea vibaya hadi tra wanateka watu siku hizi si hayo ni mazoea mabaya. Mama tembeza fimbo mama anzisha task force ya kutandaza mboko nakuhakikishia maza ukifanya hivyo kutakuwa na total nidhamu
 
Back
Top Bottom