Hivyo viwanda 4000 vilivyojengwa awamu ya 5 mbona sivijui, nafahamu kiwanda cha Dangote tu cha awamu ya 4

Hivyo viwanda 4000 vilivyojengwa awamu ya 5 mbona sivijui, nafahamu kiwanda cha Dangote tu cha awamu ya 4

Kimbakuli

JF-Expert Member
Joined
Jul 11, 2013
Posts
408
Reaction score
435
Kelele nyingi sana zilipigwa kwamba kuna viwanda vingi vilijengwa awamu iliyopita lakini hivyo viwanda mbona hutuvifahamu au ilikuwa ni habari ya guantity sio quality!

Kiwanda kimoja tu cha kuzalisha saruji cha tajiri Dangote kilichojengwa awamu ya mkwere kule umakondeni si tu kinajulikana Tz bali hata nchi jirani wanakifahamu, malori zaidi ya elfu1yaliletwa kwa ajiri ya kusupply saruji ndani na nje ya nchi, Vijana kutoka ndani na nje nchi walifurika Mtwara kufukuzia ajira, vyumba vya kupanga vilipanda sana kwa sababu ya demand kuwa kubwa.

Kifupi kiwanda hiki kilileta positive effect kubwa sana pale Mtwara Mikindani, sasa hivi viwanda elfu4 vya kayafa mbona sivifahamu au tukiviunganisha vyote thamani yake ndo tunapata kiwanda kimoja cha Dangote.

Jifunze kitu apa, acha kupiga kelele nyingi sana kuhsu ulichofanikiwa instead acha ulichokifanya kiongee chenyewe na watu watakusifu tu.
 
Una mtazamo hasi sana juu ya maendeleo na inaonekana unadharau juhudi za watu hasa wenye mitaji midogo kwamba hawawezi
 
Mkoa wa Pwani vipo vipo Bwashee! Hofu yangu ni hiyo idadi tu. Ila viwanda vimeongezeka. Na siyo wakati wa magufuli tu kama Mataga wengi wanavyo taka kutuaminisha!

Ni kuanzia enzi za JK, kuna viwanda vingi tu vimejengwa mkoa wa Pwani. Kuanzia vya nondo, tiles, nk.
 
Kelele nyingi sana zilipigwa kwamba kuna viwanda vingi vilijengwa awamu iliyopita lakini hivyo viwanda mbona hutuvifahamu au ilikuwa ni habari ya guantity sio quality!..
Huku mtaani kwetu wenye cherehani 4 na kuendelea ni wengi tu mbona huko kwenu vipi?
 
Kelele nyingi sana zilipigwa kwamba kuna viwanda vingi vilijengwa awamu iliyopita lakini hivyo viwanda mbona hutuvifahamu au ilikuwa ni habari ya guantity sio quality!...
Inategemea sana na maana yako ya kiwanda. Wengi hutegemea vile viwanda vya industrial revolution age ambapo kiwanda kinakuwa kiko kwenye eneo la zaidi ya eka moja na moshi unafuka kwenye majengo yake. Lakini viwanda vingi vya age hii huwa viko ndani ya plot moja tu na wala havitoi moshi kabisa.
 
Umeuliza swali ili ujibiwe lakini aya yako ya mwisho inaonesha ujuaji wako kuhusu ulichokiuliza.
 
Jaribu kum..cc.. mwigulu atupe takwimu
 
Enzi za Magu uongo na kupika takwimu ndiyo kulitawala. Lakini baadaya muda waliamua kuachana na sekata ya viwanda. Waliacha hata kuvizungumzia. Natumaini mama ataongea vizuri na Dangote.
 
wew shilole .. Njoo kibaha nikuoneshe viwanda.. Vijana wengi wameajiriwa huko.. Acha mipasho tembea uone.
 
Madanguro then
Najua hujawahi kununua kitu chochote kwenye maduka ya marekani, lakini sisi wengine tumeshaunua nguo na viatu ambavyo ni Made in Tanzania. Sasa kama wewe akili yako huwa inakutuma kwenye madanguro basi utapata unachotaka kununua. Waenda madanaguroni huwa ni wepesi sana wa kutaja madanguro kama sehemu ya biashara !!
 
Viwanda elf4 kwiooo labda vya kushona barakoa na mifuko ya kubebea sukari.

Ila vilivyopo vyoote ni vya mzee Msoga
 
Najua hujawahi kununua kitu chochote kwenye maduka ya marekani, lakini sisi wengine tumeshaunua nguo na viatu ambavyo ni Made in Tanzania. Sasa kama wewe akili yako huwa inakutuma kwenye madanguro basi utapata unachotaka kununua. Waenda madanaguroni huwa ni wepesi sana wa kutaja madanguro kama sehemu ya biashara !!
Ni kweli
 
Unazungumzia viwanda vya kulipwa 3500, 5500 mpaka 6300 kwa siku? Unaingia saa 1:30 unatoka saa 12:30 jioni. Serikali inabidi iangalie malipo ya wafanyakazi. Mfanyakazi anatakiwa alipwe 10,000 kwa siku.
Dumu la rita 5 la mafuta ya kupikia lilikuwa 15,000 ila sasa ni 25,000 mpaka 30,000. Malipo ni yale yale
wew shilole .. Njoo kibaha nikuoneshe viwanda.. Vijana wengi wameajiriwa huko.. Acha mipasho tembea uone.
 
Acha longo longo, viwanda 4000 viko wapi? Yaani mfano: Dar 100 viko Mbagala, Kigamboni etc, Rukwa 50 vilivyoko...., Katavi 70 etc etc
 
Awamu ya tano ilikuwa ni awamu ya propaganda tbc ilifanya Kazi nzuri Sana.Jambo moja lilitangazwa mara elf
 
Lilikuwa linapenda sifa tu ndio maana lilitaka kuzindua kila kitu hadi vyoo vya stendi
Alikuwa anapenda kuzungumza na wananchi. Huwezi Kila Mara kuzungumza na wananchi.
Wakati mwingine unahitaji sababu ya kufanya hivo.
Nadhani uzinduzi Ni miongoni mwa fursa alizotumia kuzungumza nasi.
 
Back
Top Bottom