Hizi bahati nasibu tunajiridhishaje?

ibanezafrica

JF-Expert Member
Joined
Oct 23, 2014
Posts
7,261
Reaction score
6,553
Yaonyesha wazi serikali imebariki hizi bahati nasibu zinazotamba kwenye baadhi ya redio hapa nchini.

Watu kwa maelfu wanavutiwa na watangazaji kucheza michezo hiyo ambapo kima chake ni shilingi alfu moja na mtu anaweza cheza kwa kadri mara nyingi awezavyo.

Kila kukicha hii michezo inazidi kushaamiri kwa kasi katika vituo vya redio,Ingependeza bodi ya michezo ya kubahatisha nayo itoke mbele ituaminishe kuwa michezo hii ni salama,vinginevyo kwa sisi wengine tunashindwa kuelewa tofauti ya ile michezo iliopigwa marufuku ya 'Upatu', 'Deci' na hizi bahati nasibu zilizofumuka.

La msingi hapa wananchi wajiridhishe hasa pale inapofikia kumtangaza mshindi,kwanza hawasemi au kuonyesha mshindi anapatikana vipi?kifaa gani wanatumia?na je kifaa hicho walipewa na watu wa bodi ya michezo hii au ni chombo chao?ni nani anae kihakiki kila mara,kabla na baada ya draw?

Vipi tutawaamini watu wa redio ambapo wao wanatumia sauti tu kutuaminisha bila wengine kuwaona?
Hawa watangazaji mbona wanajitahidi kuvutia sana watu wacheze hii michezo,siri gani ipo nyuma?wao wanafaidika na nini?

Je, hawa watangazaji wanafuata vigezo na masharti ya michezo ya kubahatisha?kuwa wao au ndugu,jamaa zao hawashiriki kucheza, lakini uhakika uko wapi kwamba hawa washindi wanaotangazwa hawana connection/uhusiano na watangazaji?tutaaminije?

Hii kitu kwa kweli bado haija kaa sawa, zaidi ni kuzidi kuwakamua watu masikini ambao wana suffer na hali ngumu ya maisha ya sasa kwa kuwapa matumaini kuwa wacheze kwa wingi watashinda!si sawa!otherwise hizo pesa (faida) zipatikanazo zote ziende kujenga madarasa na vituo vya afya,tuone kama wataendelea.

Nadhani Ufafanuzi wa kina unahitajika kwa umma kuhusu mchezo sio tu kukimbilia kumtangaza mshindi na kuwavuta watu wacheze.na pengine mapato yao yaanikwe tujue pia na serikali inanufaika vipi katika revenue.
 
Hujaambiwa ubeti. Ni njaa zako na tamaa zako ndio mtaji wao. So kama huna imani achana nao. Sio lazima ubeti hujashikwa mkono.
Sema hongera kwa wazo la uwazi (transparency)
 
Zinasajiliwa na Gaming Board of Tanzania iliyoanzishwa Mwaka 2003 kwa Sheria husika, michezo hii ilianza kuhalalishwa mwaka 1967.

Hata hivyo, michezo hii pamoja na kuhalalishwa kwa mujibu wa sheria inasalia kuwa kamali iliyoharamishwa na dini zote tunzoziamini hapa Tanzania yaani Uislamu, Mashahidi wa Yehova, Hindu, Budha, na Ukristo.

So CHEZA at your own risk. Ukiecheza huioni pepo, wewe ni Jehanamu moja kwa moja.

Kalomo mfyeto
OVA
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…