kumekuwa na hizi betting mashine nyingi mitaani ambako nimeona watoto na vijana wetu wameona kama ni sehemu zao za ajira.Kwangu mimi nimeona kama ni bomu linalosubiri kulipuka kwani limewafanya watoto wetu kuwa wavivu na kuona hiyo kama sehemu ya ajira.kibaya zaidi watoto wenye umri wa chini ya miaka 18 yaaani walioko sekondari wamekuwa ndio wateja tena wamekuwa wezi ili kutafuta pesa ya haraka.Kinachonisikitisha zaid hakuna hatua zozote zile serikali imechukua kuwalinda watoto wetu.Niliwahi kulalamika kuhusu bodaboda wengi wakasema eti ni ajira lakini hebu piga hesabu mtaani kwako kuna vilema na vifo vingapi vya bodaboda.Wakuu tuchukueni tahadhali tutapoteza vijana