Mindyou
JF-Expert Member
- Sep 2, 2024
- 1,869
- 4,877
Wakuu,
Takriban siku 2 zilizopita Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) ilipokea msaada wa dola milioni 9 za Marekani (takriban shilingi bilioni 24.5) kwa ajili ya kuboresha huduma za hali ya hewa.
Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa TMA, Jaji Mshimbe Bakari, alitangaza msaada huo jijini Dar es Salaam ambapo alidokeza kuwa fedha hizo zitatumika kuimarisha miundombinu ili kufanikisha upatikanaji bora wa data za hali ya hewa.
Ukiangalia kwa umakini Dola Milioni 9 (Bilioni 24.5) ni pesa nyingi sana na hii inaonesha ni kwa kiasi gani Marekani imejikita katika kuhakikisha huduma za hali ya hewa Tanzania zimeboreshwa. Lakini je kwa nature ya taasisi zetu ambazo mara nyingi zimejaa rushwa na ukiritimba, je fedha hizo zitasaidia kweli mamlaka hiyo kutatua tatizo la mabadiliko ya tabia ya nchi?
Nauliza hivyo kwa sababu, katika kauli yake wakati anapokea pesa hizo mapema wiki hii, kauli ya Jaji Mshimbe Bakari ilikuwa kama haijajitosheleza. Jaji Bakari alidokeza tu kuwa ufadhili huo utaimarisha juhudi za kutoa taarifa za hali ya hewa za hali ya juu nchini na pia aliwaomba wananchi wasipuuze taarifa za TMA.
Hakuongelea namna ambavyo pesa hizo zitatumika including, kuweka mpango mkakati au kuorodhesha ni kitu gani ataweka kama kipaumbele.
Je fedha hizo zote zitasaidia kusaidia tatizo la mabadiliko ya tabia ya nchi, tatizo ambalo kwa sasa linasababisha mafuriko na kuongezeka kwa joto hapa Tanzania?
Soma pia: TMA: Mvua za El-Nino kuendelea hadi Aprili 2024
Haya ni maswali ambayo yanafaa kupatiwa majibu especially ukizingatia kwamba pesa hizo ni nyingi.
Nawasilisha!