Lucas Mwashambwa
JF-Expert Member
- Jul 28, 2022
- 28,722
- 20,610
Ndugu zangu Watanzania,
Nimepata na kupokea Maswali Mengi sana kutoka kwa watu mbalimbali mitaani kuniuliza juu ya sababu ya Mzee Omary Mchengerwa Baba Mzazi wa Mheshimiwa Waziri wetu wa TAMISEMI Mheshimiwa Mohamed Mchengerwa Kuzikwa Makka ambako ndiko alikofia.
Nimeulizwa maswali haya siyo kwa sababu mimi ni Mwana Familia au msemaji wa Familia ya Mzee Mchengerwa au Msemaji wa Marehemu. Nimeulizwa Maswali hayo hususani na wapinzani hasa wana CHADEMA ambao wanafahamu mimi ni mwana CCM kindakindaki .Japo kifo hiki cha Mzee wetu siyo kifo kinachohusiana na maswala ya kisiasa na wala mambo ya kifo cha Mtu hayapaswi kuchanganywa na siasa au itikadi.
Kila mmoja anafahamu kuwa kwa uwezo wa kifedha na kiuchumi wa Familia ya Mzee Mchengerwa isingeweza kushindwa kusafirisha Mwili wa Marehemu kuja Kuzikwa hapa Nchini. Hivyo ni wazi hajazikwa huko kwa sababu ya kifedha.
Sasa kwanini Kazikwa Huko? Kwanini Kazikwa Huko saa chache tu baada ya kufariki au siku chache baada ya kufariki?
Haya hapa chini ndio Majibu kulingana na mila , desturi na utamaduni wa waislamu na kiislamu.
Ni Hivi Mji wa Makka Ni mji Mtukufu na wenye kuheshimika na ndoto ya kila muislamu aliyepo mahali popote pale Duniani na aliyeishika vyema Dini yake kufika mahali hapo walau mara moja tu katika Maisha yake ya hapa Duniani. Ni ndoto ya kila muislamu kufika hapo ,ni tamanio la kila muislamu kukanyaga ardhi ya eneo na mji huo,ni kiu ya kila muislamu mwenye Pumzi na afya njema kufika na kukanyaga ardhi na udongo Wa Makka.
Kwa sababu ya Utukufu na heshima ya Mji huo. Kila Muislamu anatamani hata ikitokea akifa basi azikwe katika Mji Huo. Kila Muislamu anatamani mahali hapo Ndio pangekuwa Makaburi ya waislamu Wote Duniani kupelekwa na kuzikwa mahali hapo kama ingewezekana.
Kwa hiyo Basi ikitokea Mtu Amekwenda katika Ibada ya Hija mahali hapo na kwa Bahati Mbaya akapoteza Maisha na kufia katika Mji huo mtukufu na mtakatifu .Basi hawezi akachagua kwa kuacha wosia au ujumbe wa kurejeshwa kwao au katika Nchi yake kama ilivyotokea kwa Mzee wetu Omary Mchengerwa. Ni lazima atataka akiwa amekufa Azikwe mahali hapo.
Soma Pia: Waziri wa TAMISEMI Mohammedi Mchengerwa Amefiwa na Baba Yake Mzazi Akiwa Ibadani Makka Na Atazikwa hukohuko Makka
Lakini Pili ni utamaduni na kawaida na desturi ya Muislamu kuzikwa mahali au Nchi au Mji au Eneo alikofia bila kusafirishwa umbali mrefu.Ikiwa tu kama eneo alikofia kuna waislamu wanaoweza kumfanyia taratibu zote za kumzika muislamu .yaani kupewa haki zote za Kuzikwa kiislamu.
Je Haki Hizo ni Zipi? Taratibu Hizo ni Zipi? Haki na taratibu hizo ni kwanza Kuoshwa kwa Mwili wa Marehemu,Pili ni Kuvikwa Sanda kwa Mwili wa Marehemu,Tatu ni Kuswaliwa kwa Marehemu na Mwisho ni Kuzikwa kulingana na mila na desturi ya kiislamu.
Kwa hiyo kama eneo alikofia Mtu kuna waislamu wenye kutimiza mambo hayo .Basi Marehemu atazikwa eneo au nchi hiyo aliyofia pasipo kuhitajika kusafirisha Mwili.
Mwisho wengine wakaniuliza mbona amezikwa kwa haraka sana. Hilo swali nazani ni jepesi sana kwa sababu siyo geni kwa hapa Nchini kwa watu wengi pale inapotokea kafariki Muislamu
. Ni utamaduni wa waislamu kuzika muda mfupi au siku chache isiyozidi hata siku moja au mbili tangia kufa kwa Mtu. Ili mtu huyu akapumzike na kuanza kuhesabiwa na kulipwa Haki kulingana na matendo yake aliyoyatenda hapa Duniani.
Msisitizo ni kuwa Mimi Mwashambwa Lucas sijasema mimi ni msemaji wa Familia,wala sijasema nimetumwa na Familia ya Mzee Mchengerwa. Nimeelezea kulingana na taratibu za wenzetu. Kwa hiyo msianze kutukana matusi na kunitusi.
Ni katika kupeana tu Elimu.
Asante pia kwa Chifu Mkuu mwana Jamii Forum kwa Elimu hii.
Kazi iendelee, Mama Ametufikia na kuwafikia watanzania kwa utumishi wake uliotukuka wa kugusa Maisha ya watanzania wanyonge wasio na Sauti.
Lucas Hebel Mwashambwa, Mama ANATOSHA kuendelea kuliongoza Taifa letu kwa muhula wa pili.