Jodoki Kalimilo
JF-Expert Member
- Feb 12, 2012
- 12,559
- 11,180
Mi nalipiaga tu ila nakuja pandisha bei kwa ninaowauzia basi. Yaani kadiri TRA anavonikamua ndo na mie ninavohamishia burden ile kwa ninaemuuzia gari. sina muda wa kuhoji
Wasiliana na TRA wenyewe watakupa majibu ya hio kitu. Namba za simu na huduma kwa wateja zipo kwenye website yao www.tra.go.tz
Hizo formula tu zinahitaji jitihada ya ziada kuzielewa na kuzifafanua, sasa kwa wabunge wetu ambao ni wazee wa imepita bila kupingwa so long mswada umeletwa na serikali hapo ndio inakuwa kasheshe ukichanganya tena ni mambo ya hisabati wataishia kusema haya ni mambo ya kitaalamu, kiukweli kodi kwa Tanzania inalipwa na watu wachache kwa niaba ya wengine na sidhani kama serikali ingebuni vyanzo vingine vya kodi hili tatizo lingeendelea
Unajua mkulu hizi sheria zinaanzia kwenye kamati za kisekta, wizarani hatimaye zinaenda mpaka bungeni... sasa tukiwalaumu wabunge tutakuwa tunawaonea kwa sababu wenyewe (wengi wao si wataalam wa mambo mbalimbali).... na pale bungeni hawapati muda wa kupitia vipengele vyote kwa undani.... ndiyo maana wanasema tu ndiyoooo.... na hapo waheshimiwa wabunge wakiingiza ushabiki wa kivyama hali inakuwa mbaya zaidi, maana wanaunga mkono hoja bila hata kuitafakari na kuipima ilimradi tu inatoka chama chake.....
Wasiliana na TRA wenyewe watakupa majibu ya hio kitu. Namba za simu na huduma kwa wateja zipo kwenye website yao www.tra.go.tz
uliyoyaongea yana maana sana.
Yani kitu kipo "compounded" badala ya kua from base. Maana ni kua tax base haijulikani.
Ni sawasawa ukatwe sdl kwenye mshahara, kiwango kinachopatikana kijumlishwe tena kwenye mshahara ukatwe paye, wizi mtupu huu.
Cha ajabu kingine formula zao zina mikwara mingi tu badala ya kua straight. Hayo yote ni kutengeneza mazingira ya kula.