Hizi Marathon zinaendeshwa chini ya mamlaka gani na kwa udhibiti wa nani?

Hizi Marathon zinaendeshwa chini ya mamlaka gani na kwa udhibiti wa nani?

Linguistic

JF-Expert Member
Joined
Mar 16, 2021
Posts
3,669
Reaction score
8,268
Wakuu habarini za machweo.

Kwa muda mrefu nimeona utitiri wa hizi mbio zinazoitwa za marathon ambazo zimeibuka kwa kasi sana kipindi.

Sina upingamizi na hizi mbio zao ila ninachotaka kukisema ni kwamba regulation ya hizi marathon is very important.

Zinaendeshwa chini ya mamlaka gani na kwa udhibiti wa nani?

Halafu katika mbio kama hizi ambazo si za kimichezo, lazima kuwe na makundi: K.M. Umri na jinsia ila kwenye hizi za nina marathon naona wameweka jinsia tu.

Ni maoni yangu.

Screenshot_20210603-080441.jpg
Screenshot_20210603-080429.jpg
 
Iyo ni shughuli maalumu kwa ajili ya kusaidia wagonjwa wafanyiwe upasuaji na zinahitajika milioni mia 8 kama sijakosea nikusaidia wenye matatizo ya uti wa mgongo pia sio lazma ushiriki kukimbia mchango wako wa fedha ni muhimu zaidi. Wahusika wakuu watakueleza zaidi
 
Asilimia kubwa ya Haya Mashindano, ni Kujitafutia Pesa kwa migongo ya Riadha.

Udhaifu wa Shirikisho la Riadha Tanzania ndilo lililoletea hayo Yote.

Shirikisho halina Ratiba ya Mwaka hadi muda huu.

Viongozi wengine wapo hata vyeti hawana, je wataweza kusimamia katiba ya chama?
 
Hapo umesema Kiongozi!

-Hakuna malengo yoyote.
-Hakuna faida Kwa jamii baki ya washiriki kulipa kiingilio.
-Hakuna uhakiki wa mbio zenyewe.
-Na pia mbio yenyewe sio marathon isipokuwa ni 21km ambayo ni nusu ya marathon.

Ufuataji wa kanuni na mipangilio thabiti huwa ni tatizo kweli kweli.
Tutapigaje hatua kwa mambo ya kuweka plasta kwenye kidonda??
Wanaoongoza World Athletics wakiona hii italeta sokomoto!!
Haya twendeni tuu,,,,,,,!
 
Its an opportunity to mingle. Ni nafasi nzuri pia kwa SM na girls over 30 kuonekana kwa haraka.
 
Udhaifu wa Shirikisho la Riadha Tanzania ndilo lililoletea hayo Yote.

Shirikisho halina Ratiba ya Mwaka hadi muda huu.

Viongozi wengine wapo hata vyeti hawana, je wataweza kusimamia katiba ya chama?
Hili limesababisha Taifa kukosa wawakilishi wa kutosha kwenye mashindano ya kimataifa,

Mfano hai angalia ushiriki wa Tanzania kwenye mashindano ya mwaka huu hata mwaka jana, kisha linganisha na ushiriki wa wa_Kenya kwenye hayo mashindano.
 
Hizi Marathon hazijawa na effect yoyote kwenye mchezo wa riadha.
Pamoja kuwa nyingi sijaona zikizalisha wanaridha wa kushiriki mashindano makubwa kama Olympic.
 
Hizi marathon ni for fun.. ukipenda unalipia unaenda kuburudika at the same time kuchangia theme au malengo ya hio marathon..
sio “athlete talent search”
Ni kama tunavyokwenda bar kunywa mbili tatu.

Umeshushiwa na kitu kizito, nini?
 
Kuna vibali wanaomba kwa mamlaka husika.
Ni jambo zuri kuwa na hizi marathon. Kunafanya wengi hasa wafanyakazi wa maofisini kushiriki mazoezi kwa ajili ya kuboresha afya lakini kwa jamii kwa ujumla kuchangia nia ya marathon husika.
Chama au mamlaka ya mbio nchini wajiongeze wenyewe kuweka udhibiti ingawa huwa wanashirikishwa.
 
Asilimia kubwa ya Haya Mashindano, ni Kujitafutia Pesa kwa migongo ya Riadha.

Udhaifu wa Shirikisho la Riadha Tanzania ndilo lililoletea hayo Yote.

Shirikisho halina Ratiba ya Mwaka hadi muda huu.

Viongozi wengine wapo hata vyeti hawana, je wataweza kusimamia katiba ya chama?

Na udhaifu wa shirikisho ndio umepelekea wapigaji kubuni majina na kuyapachika kwenye hizi marathon.

Hebu chukulia kila kichwa kinajiandikisha kwa elfu 30, je hizo pesa huwa zinakwenda wapi?!

Ni usakala tu wa viongozi wa michezo Nchini...
 
Shirikisho la riadha limeshindwa kutumia nguvu yake kusimamia, Kama hawapewi rushwa Basi Kuna uzembe mahali...mwaka Jana walikuwa na Ratiba lakini mwaka huu kila mtu anahitangazia mbio yake akisijikia..Je mbio hizi zinavigezo na usalama unaohitajika? Wanalipa Kodi ? Mbio hizi Ni kunufaisha watu au jamii Kama wanavosema...?

Sent from my Infinix X657 using JamiiForums mobile app
 
Ni sawa na ukeshapo mwenge...KIGOGO2014 anakwambia full kudu masitu
 
wanaoshiriki na kupata medani sijawahi kusikia wameshirki haya ambayo kuwakilisha nchi wakarudi tz na kuvishwa mashada
 
Back
Top Bottom