Hizi mila nyingine bwana we acha tu

Mr Hero

JF-Expert Member
Joined
Jun 11, 2015
Posts
5,540
Reaction score
7,455
Basi wiki iliyopita jirani yangu alipatwa na msiba huko kijijini kwao, ikabidi nimsindikize kwenda kuzika, utaratibu wa kuzika baada ya kuzika kwa mila yao, mzee wa kimila hutangaza nani ataefatia kufa,
Sasa bwana tumeshazika na mzee alisimama akatutazama!! Kakohoa kidogo kuweka sauti sawa.
Ndugu zangu wanakijiji wenzangu naomba nimtambulishe mtu ataefata kufa baada ya huyu tuliemzika,
Mmhh watu wote matumbo moto,
Mzee akasema mtu wa Kwanza kutoka hapa ndio ataekufa baada ya huyu,
Nakwambia huwezi kuamini tuna siku ya 3 makaburini hapa tunazunguka zunguka tu pamoja na mzee mwenyewe!!!
 
heheheeeeeee. kwa hiyo mnaona bora mfe kwa njaa kuliko kuwa wa kwanza kufa?
 
Hatari sana, nimelazimika kushea na washkaji hapa, ni kicheko balaaaaaaaaaaa
 
Ningekuwepo mm kwa imani yangu niliyoko nayo, baada ya huyo mzee kumaliza neno la mwisho naamsha saaa hiyo hiyo
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…