Jaman kuhusu maji Kata ya Nyampande Wilaya ya Sengerema Mkoa wa Mwanza ni janga kubwa, tuna mabomba ila maji ni kitendawili, Waziri kaja Mwanza jiji, viongozi wetu wanajua lakini bado hawajatatua hii kero.
Tangu mradi uanzishwe, maji yanatoka kwa mwezi mara moja au mbili tu na baadhi ya vitongoji hawapati maji kabisa.
Mfano Mtaa wa Mission na Mtaa wa Robo hatupati maji kabisa. Baadhi ya wateja wameamua mamlaka waje wachukue mita zao.
Mradi ulianzishwa wa kata moja ila kwa sasa inahudumu zaidi ya kata 3 nadhani ndio sababu ya mradi kuzidiwa, kata zilizoongezeka ni Tabaruka na Kasungamile kwa baadhi ya vijiji vyao ambavyo ni Busulwangiri, Mayuya na Ilekanilo.