Hizi ndio hoja zangu kwenye sakata la ndege inayotajwa kubeba watalii

Hizi ndio hoja zangu kwenye sakata la ndege inayotajwa kubeba watalii

Escrowseal1

JF-Expert Member
Joined
Dec 17, 2014
Posts
4,618
Reaction score
4,605
Wadau wa utalii wamejitahidi sana kutetea hoja ya matumizi ya raslimali za nchi.

Hoja zangu ni hivi, inatia moyo kuona wananchi wako macho juu ya rasilimali za Taifa tofauti na huko nyuma.

1. Kila mtanzania anajua kuwa baadhi ya viongozi walishawahi jihusisha na usafirishaji wa wanyama hasa twiga, hoja ambayo serikali jaijawahi ku clear.

2. Hunting block inayopigiwa kelele ambayo BBC ilishawahi kuandika kuihusu kuwa kuna mtandao wa simu unaokukaribisha uarabuni ndani ya hifadhi ya nchi yetu pia haijawahi kufafanuliwa na serikali kwamba imekaaje.

2. Majibu yanayotolewa na ama na KADCO, Wizara husika na Msemaji wa Serikali, wananchi wanatoa hoja kuwa hayafanani.

4. Tunapohamia ku deal na Middle East countries kwenye masuala ya uchumi hasa kwa nchi zetu za Kiafrika wananchi hatuna budi kujivika uendawazimu kutokana na tabia za hizo nchi kutoa rushwa sasa zikichanganya na tabia za Kiafrika.

Sina uhakika chemical reaction itakayolipuka, Waziri amesema Watanzania tuwe wazalendo; mi nadhani hakuna uzalendo unaozidi kuwa na tabia ya kuwa na wivu na rasilimali zinazotuhusu. Afrika tumekuwa let down na viongozi wetu big time.

Screenshot_20230115-001414.png
 
Back
Top Bottom