Mindyou
JF-Expert Member
- Sep 2, 2024
- 1,869
- 4,877
Wakuu,
Hivi karibuni, Shirika la Umoja wa Mataifa UNESCO limetoa ripoti mpya inayoelezea kwa undani idadi ya watoto ambao wanastahili kuwepo shuleni lakini kwa sababu tofauti tofauti hawapo shuleni.
Soma pia: Ukatili unaofanyika kwa watoto wa shule binafsi ya EXPERANCIA (Sengerema)
Kulingana na ripoti ya Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO), watoto na vijana milioni 244 wenye umri wa miaka 6 hadi 18 duniani kote bado hawajapata elimu, na takriban shule 14,300 zimefungwa katika nchi 24 za Afrika kufikia Juni 2024 kulingana na Baraza la Wakimbizi la Norway (NRC).
Ripoti hiyo imezitaja nchi kama Burkina Faso, the Democratic Republic of Congo, Cameroon, Chad, Nigeria na Niger kama nchi zinaozoogoza kwa kuwa na watoto wengi wasioenda shule huku umasikini ukitajwa kuwa ni sababu kubwa inayopelekea watoto kukosa kwenda shule.
And yes Tanzania pia ipo.
Kulingana na ripoti ya UNESCO hizi ndio nchi zinazoongoza kwa kuwa na watoto wengi wasioenda shule Afrika:
Kwa hiyo hapa Tanzania kuna watoto Milioni 6 hwaendi shule, hawa watoto huwa wanafanya nini huko mitaani kama hawaendi shule? Elimu si bure?

- Nigeria – 18.18M
- Ethiopia – 11.1M
- Tanzania – 6.42M
- DR Congo – 6.17M
- Sudan – 5.6M
- Niger – 5.5M
- Uganda – 4.9M
- Angola – 3.9M
- Burkina Faso – 3.4M
- Mali – 3.1M