Wahenga walisema elimu ni ufunguo wa maisha, ipo wazi na hilo halipingiki kwasababu ili mtu afanye mambo kwa weredi ni lazima awe na elimu au ujuzi wa kutosha kuhusu jambo analofanya.
Watu wengi katika jamii hasa za kiafrika hawajaipa kipaumbele elimu, jambo linalopelekea kufanya mambo tofauti na ulimwengu wa sayansi na teknolojia unavyoenda.
Mambo yanayofanyika katika jamii lakini yamepitwa na wakati ni kama kukeketa wanawake, ndoa za mitala, Imani potofu, na unyanyasaji wa kingono kwa jinsia zote yaani kwa watoto wa kike na wa kiume.
Sababu zinazopelekea uwepo wa mambo ambayo yanapelekea unyanyasaji wa kijinsia yapo mengi lakinj miongoni mwa hayo ni ukosefu wa elimu kwa wanajamii kuhusu mila potofu ikiwemo ukatili wa kijinsia.
Sababu nyingine ni adhabu zilizopo kuonekana ni nyepesi kulingana na ukubwa wa kosa, baadhi ya watu wameendelea kufanya vitendo vya ukatili wa kijinsia kwasababu adhabu ni nyepesi kwao ndio Maana matukio hayo yameidi kuongezeka.
Imani za kishirikina, sababu nyingine inayochongia uwepo wa ukatili wa kijinsia ni mila potofu mfano kuendekeza Imani za kishirikina kama kwenda kwa waganga ambao wanahusika kuwadanganya wanaume kuwaingilia kinyume na maumbile watoto wao ili wapate utajiri.
Utekelezaji mbovu wa adhabu zilizopo, inawekana Sheria zilizopo ni kali na zinapinga vitendo vya ukatili wa kijinsia, lakini usimamizi mbovu katika kutekeleza adhabu ndio Sababu nyingine inayochongia matukio hayo kuendelea kuwepo hasa maeneo ya vijijini.
Uelewa mdogo wa jamii juu ya athari za ukatili wa kijinsia, watu wengi wanafanya matukio ya unyanyasaji wa kijinsia kama kukeketa wanawake kwasababu hawana uelewa juu ya athari za ukeketaji kwahiyo elimu zaidi inahitajika Ili kuikomboa jamii.
Kukosa hofu ya Mungu, sababu nyingine inayopelekea matukio ya ukatili wa kijinsia kuendelea siku hadi siku ni ukosefu wa elimu ya dini ambayo ingesaidia wanajamii kuwa na hofu ya kutenda matendo hayo kwasababu ni kinyume na Mungu kwahiyo elimu ya dini inahitajika pia.
Ukosefu wa elimu ya saikolojia, katika jamii zetu za kiafrika elimu ya saikolojia haijapewa kipauumbele hali inayochongia ukatili wa kijinsia, mfano baba amegombana na mama anaona suluhisho ni kumpiga na kumjeruhi lakini kama angekuwa na elimu ya saikolojia ingemsaidia kutambua anayofanya sio sawa.
Kwahiyo ili kuepukana na matatizo yanayotokana na ukatili wa kijinsia ni lazima serikali ishirikiane na taasisi za kidini na za kiraia kukemea vitendo hivyo na kutoa elimu mijini na vijijini ili jamii iepukane na matendo hayo yanayochafua taswira ya nchi.
Penye nia pana njia na kila changamoto haikosi utatuzi niwaombe wananchi wenzangu tushirikiane na serikali kukemea matendo hayo ya ukatili wa kijinsia na pia kuwalinda watoto wetu ili watu wenye nia mbaya wasiwarubuni na kuwaharibia maisha.
Mwisho nichukue nafasi hii kuwaasa wanajamii kushiriana kwa pamoja katika kupeana elimu sisi kwa sisi ili tuilinde jamii na kulinda kizazi chetu kikue katika maadili bora ya kumpendeza Mungu.

Upvote
2