Hizi Ndizo Nasaha Nilizopewa na wazee Mimi Kama Kijana wa Kiume! Itakufaa sana wewe Mwanaume!

Ryzen

JF-Expert Member
Joined
Dec 6, 2012
Posts
7,301
Reaction score
8,706
Juzi Niliitwa na Wazee wangu wa Ukoo, Nikiwa kama Kijana Mdogo Msomi ambaye Nimekuwa Kiongozi wa Kimila wa Vijana.. Pia walikuwa wameita Vijana wengine kama 10 wa ukoo ..



Kufika Pale tulisalimiana na tulipata Kidogo Pombe ya Kienyeji.. Kisha wazee wakatujuza kwamba sisi sasa tumekuwa Vijana wakubwa, Muda wowote tunaweza Kuoa na tukawa na Familia zetu..

Wazee wakatujuza kuwa lengo la kutuita Pale ni Kutuasa Jinsi Maisha yanavyoenda hasa Katika Upande wa Familia.. na Maisha kwa Ujumla..



Naamua Kushare Nasaha Hizi Pamoja Nanyi Wanaume wenzangu wa JF



Hizi Ndizo Zilikuwa Nasaha zao!

  • Kamwe usioe mwanamke mzuri sana Kupindukia, Hafai kuwa Mke si kwa sababu ni mzuri bali atakuwa macho ya wengi na atakuyumbishia Nyumba yako.

  • Katika Nyumba yako Kuwe na Chumba chako na cha Mke wako.. hii itasaidia mwanamke wako kutokukushtukia siku ukipiga kimada huko nje(Wanaume hatuwezi Kuepuka Hili).. na kama wewe ndo unataka game kwa mke mpaka umuite Chumbani kwako.. Tofauti na hivyo mke hatakiwi kuingia chumbani kwako..

  • Usitabirike kwa Mwanamke, Ratiba yako ya kurudi nyumbani isijulikane, Kuna siku saa 1, kuna siku saa 5 kuna siku hata saa 7.. lakini kamwe usilale nje ya kwako bila sababu maalum.

  • Ikitokea mke wako akapata tetesi za wewe kuwa na kimada.. kamwe usikubali na unatakiwa ugombe hata wiki nzima na umuongezee na Majukumu ili awe busy asifuatilie mambo ya kipuuzi..

  • Kamwe usimpe Mwanamke Moyo Wako, Mwanamke si ndugu yako.. ndio maana wakati unaoa wanaangalia kuwe hakuna undugu.. Asijue mali zako zote afahamu chache tu zinazostahili yeye kuzifahamu!

  • Ukiona Dalili za mke wako kutoeleweka.. Mali zako ambazo hazijui waambie ndugu zako au wanao, kwa sababu Kifo kipo saa yoyote!

  • Kamwe usinywe pombe sehemu moja tu, watu wengi wameangamizwa kwa pombe, na ikiwezekana watu wasijue kama unakunywa pombe hata mke wako na hata ikibidi Pombe zako zinywe Chumbani kwako..

  • Kamwe usifanye Biashara na ndugu, Ndugu akikudhulumu ndo imepita na ikumbukwe ndugu hapelekwi mahakamani..

  • Kama una Mwanao na anafanya kazi kwako labda kwenye biashara au shamba lako Mlipe kama watu wengine, usimwache mwanao afanye kazi bure kisa tu ni ya nyumbani..

  • Hakikisha Mwanao hafuati usasa wowote, Mwanao mpe majukumu ukiona haelewi.. mpe ile sehemu ya urithi wake.. na umpe kwa maandishi ukimweleza kwamba akiitumia vibaya asigeuke nyuma na akigeuka atarudi kama kibarua na atalipwa kama kibarua wengine!

  • Kuwa makini siku zote, Hakikisha hauwahiwi kwenye meza ya Kiufundi, ukiwahiwa kuchomoka kwako ni Ngumu au unaweza usichomoke kabisa!

  • Mwanamke wa kwanza hafukuzwi isipokuwa wakati hajazaa anafukuzika na haina shida kabisa na kwa kiasi Fulani mwanamke mwenye mtoto mmoja kama haeleweki anaachika tofauti na hivyo Hapana..


Mimi..



Divine Khan
 
Huo ushauri umepatiwa na watu wanaokufaham, umekulenga wewe.

Sie tulishapewa na wazee wetu, ambao hawajapewa nao watapewa muda ukiwadia.

Kuna vitu wamekushauri mahsusi kwako sie wengine tulishauriwa tofauti.
 
Huo ushauri umepatiwa na watu wanaokufaham, umekulenga wewe.

Sie tulishapewa na wazee wetu, ambao hawajapewa nao watapewa muda ukiwadia.

Kuna vitu wamekushauri mahsusi kwako sie wengine tulishauriwa tofauti.
Tudondoshee Nondo Mkuu!, Hizi ni nasaha tunapeana tu.. Kama baba wa taifa alivyotoa Nasaha zake kwa taifa..
 
kalaga baho
 
Ushauri mwingine umekaa kikorosho korosho eti "mkeo asijue mali zako zote" huyo ni mke au kimada?
Eti "usioe mwanamke mzuri sana"
Mlifanya vibaya kupiga pombe kabla ya mazungumzo.
 
Hapo kwenye kila mtu na chumba chake (mume na mke)
 
Safi
 
nimeelewa zaidi hapo mwisho tu mwanamke mwenye mtoto mmoja anaachika
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…