Hizi ndizo sababu? Wakaka inawahusu

Tausi Mzalendo

JF-Expert Member
Joined
May 23, 2010
Posts
1,470
Reaction score
722
KWA NINI WANAUME WENGI SIKU HIZI WANAKWEPA KUOA
KAAZI KWELI KWELI!
Sasa nini kifanyike kama hizo ndizo sababu?
 
KWA NINI WANAUME WENGI SIKU HIZI WANAKWEPA KUOA

KAAZI KWELI KWELI!
Sasa nini kifanyike kama hizo ndizo sababu?


kupunguziana cost na pamoja na kutokuoa mwanamke ambaye yupo mbali na familia yako..
 
kupunguziana cost na pamoja na kutokuoa mwanamke ambaye yupo mbali na familia yako..

Kwenye bold ina maana kuoana kabila moja au ?
Kupunguzianaje costs mkuu? Ina maana mwanamke achangia mahari yake au kwenye maeneo gani? Mimi sitakubali kujinunulia nguo ya harusi lol..itabidi mchumba anunue.Vikao vya harusi gharama ni zake pia maana nasi kwetu vitakuwepo vya send off!Gharama siyo upande wa bwana tu hata kwetu zipo.
 
Unachosema Tausi Mzalendo kina ukweli kwa sehemu, gharama zimekuwa kubwa ingawa sidhani kama zinafika huko! Kwa upande wangu naona ni vzr kijana kuoa kama amempata mwenziye. Ni vzr zaidi wadada kuwa considerable kwa kujaribu kupunguza gharama zisizo za lazima kwenye hayo maandalizi, na kuacha kufanya masherehe makubwa kwa kuiga iga sherehe za wenzao, badala ya kufanya kitu kilicho ndani ya uwezo wenu!

Lakini nafikiri pia kuna sababu nyingine nyingi zinazowafanya vijana wasioe siku hizi ikiwemo kukwepa majukumu, kuchungwa, kulindwa, kufuatiliwa, kuwa tabia ya kuwa na wasichana zaidi ya mmoja kwa wakati mmoja, commitment, wengine hupendwa kutunzwa na wadada, kukosa kazi, kukosa kipato, frustration, sababu za kibailojia na mengineyo mengi!
 
Mwanaume ambaye hana uwezo hatakiwi kuoa hayo mbona yanajulikana toka zamani, sasa kipi kipya.
 
Gharama tu ndio sababu ya kutoooa au watu nao akili zao zimekaa kushoto kulia? Kwani lazima uhakikishe mji mzima unajua unaoa?
 
izo ni gharama za harusi sio ndoa bwana
mwenye shida ya ndoa anione mimi nahamia hivohivo bila harusi
sina makuu mie

Smile , basi siku zote hizi mie najua tayari u-ndoani !
Kumbe bado !
Sasa leo ndiyo nimeishajua sababu ya vituko na vibwekwa vyako coz ni nini .
Kumbe tatizo lako si la India, ukishapatiwa dawa muafack acha kukosea kunywa sumu, hata maji yasiochemshwa huwezi kosea ukayanywa.
 
ndo ivo bwana sina ndoa.sasa unanisaidiaje?
 

kabila moja au mkoa jirani na wakwenu pili kuhusu kushare cost nizile za kuwatunza ndugu zake na wako kipindi cha harusi kuliko kumuachia mtu mmoja na hilo gauni la harusi kwanini usijinunulie kumpunguzi mmeo gharama zisizokuwa na ulazima kwake..

hasa wanaongoza kwa kutolewa gharama na upande mmoja ni pale mwanamke asipokuwa na kazi ndipo inapokuwa kazi..
 

hahhah... gauni ya harusi sinunui hata kwa kiboko!
Halafu baadhi ya gharama mwanaume anajitakia mwenyewe - kuwatoa mashemeji wakajinafasi - anatafta sifa za kijinga mwenyewe.
Malazi na chakula kwa wageni na wakwe mbona kamati inatenga fungu kutoka kwenye michango.
Mi ningeshauri, wahusika wenyewe waamue aina ya sherehe wanayoitaka na kuweka kiwango chini.Tatizo waoaji wanatafuta mashindano wenyewe kwa wenyewe.
 
Mie bana nishamwambia mtu wangu sihitaji mamilolongo ya sherehe na magara kibao kwa ajili tu ya kuoana,
Km ana hela agaramikie km hana familia yangu ikishaniaga,siku ya ndoa tukishatoka kanisan tunakua tumeandaa kitafrija tu kidogo na ndugu wa karibu na marafiki zetu tule na kunywa na kupongezana hata pale hm au hotelini kitu cha masaa 2 tu tuwe tushamaliza twende zetu hane muni basi na kila mtu arudi makwao.

Haya mambo yakupeana stress na madeni kwa ajili ya siku moja wala sinaga mzuka nayo kbs!.
 
rejao akufanyii tena harusi?
 
Kwa kweli hii mada na yenyewe inaweza kuwa sababu watu kwanini wasije kuamua kuoa maana ukipiga mahesabu hayo yote? Laiti watu wasingejua u naenda tu na flow...
 
gharama tu ndio sababu ya kutoooa au watu nao akili zao zimekaa kushoto kulia? Kwani lazima uhakikishe mji mzima unajua unaoa?

ukweli umedhihiri ktk maneno yako haya, mwenye kuuhitaji na aufanyie kazi, kila mmoja ni vyema akaishi awezavyo, na si apendavyo!
 
mimi jamani marafiki ndugu na jaa samahani nataka nizoeleke kwd ndugu, halafu awe jirani yangu wa pale maskani nadhani hyo figure ita pungua
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…