Hizi ndizo sababu zinazopelekea watu kutokuoa au kuolewa

Hizi ndizo sababu zinazopelekea watu kutokuoa au kuolewa

chizcom

JF-Expert Member
Joined
Jul 31, 2016
Posts
8,680
Reaction score
18,035
Kipindi cha zamani kushuka 2000 kila jumamosi au siku za ijumaa popote upitapo lazima ukute sheree ambayo ni ndoa.

Ilikuwa ni fahali na heshima kubwa unaposikia au kuona mtu kaoa au kaolewa. Hata kunapotokea vikao au maongezi kama ujawa sehemu hii uwezi kuruhusiwa.

Jambo lilo nileta hapa kueleza haya baada ya kuona mtaani kwetu tena uswahilini karibia watoto nilio waona wanakuwa wote wamezalishwa na kuzaa yani nje ya ndoa.

Sababu zinazo pelekea haya

Utandawazi
Utandawazi umeharibu malezi ya uzao mwingi na kujikuta maadili kama ya zamani kupotea na watu kuishi wanavo jua wao.

Malezi na makuzi
Kusema kweli wazazi wa sasa hivi ni kama wanakamilisha tu yao sio wale wa zamani .hili linapelekea watoto kuwa na mambo ya ajabu.

Maisha na kipato
Sehemu kubwa vijana ujikuta wameingia kwenye mapenzi au kuzaa bila ndoa au tamaa zinazopelekea watoto wasio kwenye ndoa.kwa sababu ya mwenendo wa maisha na pesa

Hizi ndizo sababu zangu
 
Huku kwetu mbona kila jumamosi na jumapili bado sherehe zipo tena za kutosha [emoji3][emoji3]ndoa na engagement kama zote
 
kuna ukweli ndani yake sema pia sikuhizi
1.hofu ya Mungu haijatawala kama zamani nahisi inaingiliana na utandawazi kuwa kuzini imekuwa jambo la kawaida sana

2. Wanawake wengi wame elimika na wanajua haki zao, sikuhizi uwezi ukampiga mwanamke hovyo na akakuvumilia.

3. Simu, ndio utandawazi wenyewe, sikuhizi option zimekuwa nyingi, sio kama zamani kuwa utampenda uliekua nae hapo kijijini, sikuhizi kuna mitandao ya kijamii, transport nayo imerahisisha maisha mtu ku explore choices zake.

4. Hii ni ya msingi, vijana wa kiume wengi hawana ajira, zamani walikua wanalima , atapewa ardhi ataweza kuoa na kumlisha mkewe na watoto. Sikuhizi tunasoma, mtu akimaliza shule ndio aanze kutafuta kazi au biashara ndogo ndogo mpaka mambo yakae sawa sio leo, wanaume wengi wanapenda kuwa na financial freedom ndio waoe.

5. Bendera fata upepo, mazingira wanayowazunguka vijana wengi unakuta wanashauriana ujinga kama hivyo kwanini nioe wakat naweza muita tu mdada nikaishi nae ikaisha?
 
Gharama za maisha zimekuwa juu, mitindo ya maisha nayo inachangia vijana na mabinti kutokuoana. Utakuta binti anamiliki simu ya gharama kubwa halafu hana kazi ya kuweza kumpatia hela ya kununua hiyo simu lazima aogopwe na kijana asiye na uwezo wa kununua simu hiyo. Kingine ni suala la ajira kama binti ana kazi anachagua aliyemzidi kipato, ndio maana kunazidi kuwepo kwa wamama wenye familia bila baba anayefahamika yaani single mother
 
Mastaa wa kike nao wanachangia kusiwepo kwa ndoa au ndoa feki, sasa kama wanaolewa na kuachika kila mara kisa wana jeuri ya fedha, wanaigwa na wanawake wengine, unakuta staa wa kike ana watoto hata watatu na kila mtoto ana baba yake halafu anajiita single mother anaona huo mtindo wa kuzaa na mwanaume anayemtaka ndiyo fasheni, na mashabiki wake wanamuiga mitindo yake ya maisha. Viongozi wa kimila na dini ni kama wamezidiwa kuhusu maadili ya jamii juu ya suala la ndoa
 
Back
Top Bottom