NALIA NGWENA
JF-Expert Member
- Oct 6, 2016
- 10,587
- 13,425
Hakika yanga inastahili kupewa maua yake kwa hatua kubwa/viunzi vigumu ilivyo viruka nakufika hapo ilipo hakika inastahili pongezi maana imeliheshimisha taifa kwa ujumla.
Kupiga hatua kwa yanga Kuna silaha madhubuti /maridhawa zilizotumika mpaka yanga kufika hapo ambazo ni Kama ifuatavyo.
(a) Kocha na benchi lake la ufundi imara, hapa Kuna kocha wa mpira Prof Nabi, makocha wa viungo na makipa hakika wamejitahidi sana katika kuweka sawa miiili ya wachezaji wanastahili pongezi/sifa maridhawa.
(b) Video analyst (mchambuzi wa video) yanga ilimsajili huyu mwamba watu wakaanza kuleta utani, hakuna asiyejua kuwa yanga inashinda mechi za nje na ndani pia bila wasiwasi wowote huyu video analyst anaifanya kazi yake vyema kabisa.
(C) Uwekezaji/usajili wa wachezaji Bora , hapa yanga naipa eco katika kusajili quality players hakika matunda ya wachezaji Bora tunayaona, huwezi kuwa Bora kimataifa Kama hausajili wachezaji Bora hakika hii inaleta mafanikio katika timu.
(d) Viongozi wasioteteleka, uongozi huu ni tofauti na uongozi uliopita kuwepo kwa damu changa hakika inachangia kuleta mawazo chanya/ubunifu mujarabu ndani ya timu.
Hakika engineer Hers na wenzake wanaupiga mwingi mnoo mpaka una mwagika.
NB: Yanga inaliwakisha vizuri taifa na inafuta ile aibu ya timu fulani iliyopigwa faini kwa tuhuma za kichawi na kuchoma uwanja.
Sent from my Infinix X657 using JamiiForums mobile app