Hizi ndo sababu za mwanaume/kijana kupoteza uwezo wa kuzaa-kutopata mtoto

Hizi ndo sababu za mwanaume/kijana kupoteza uwezo wa kuzaa-kutopata mtoto

mwekundu

JF-Expert Member
Joined
Mar 4, 2013
Posts
21,859
Reaction score
19,736
HIZI NDO SABABU ZA MWANAUME/KIJANA KUPOTEZA UWEZO WA KUZAA-KUTOPATA MTOTO

Vijana ambao bado wana mawazo ya kuongeza familia wakati mwingine hushiriki katika tabia fulani hatari si tu kuhatarisha afya zao lakini afya ya manii zao pia.
Wanaume watu wazima vilevile wakati mwingine hushiriki tabia ambazo haiwezekani, kumpa ujauzito mwanamke.

Daktari wa familia, Dk Toun Agbaje, anasema, kwa ujumla, afya ya manii inategemea sababu kuu tatu - wingi, ubora na motility (harakati). Anasema mtu ili aweze au awe na uwezo wa kumpa mimba mwanamke ni lazima awe na uwezo wa kutoa mbegu(sperms) zaidi ya milioni 15 kwa kila mshindo mmoja(1-ejaculation)
Ni kwa jinsi gani mwanaume anaweza athiri mbegu zake?

1.Mtindo wa uvaaji . Je, umeona style dressing miongoni mwa vijana? Imekuwa kawaida kwa vijana kuvaa underwears nyingi na zinazowabana(kiduku style).Profesa wa Uzazi Endocrinology, Oladapo Ashiru, anaonya kuwa uvaaji wa chupi nyingi na nguo za kubana huongeza joto la korodani na kusababisha kupunguza uzalishaji wa mbegu. Anaeleza kwamba korodani hutegemea joto la nje ya mwili,na huzalishwa katika ujoto wa 1-2 digrii centigrade chini ya joto la mwili 37 ° C.(ndo maana korodani zinaninginia nje ya mwili-special adaptation)

2.Uwekaji wa laptop(computer pakato) juu ya mapaja(lap) wakati wa kufanya kazi
Watafiti katika Chuo Kikuu cha New York stony broke Brook kusema, "Kuna uwiano wa moja kwa moja wa kuongezeka joto la korodani hadi hadi kufikia 35 ˚ C ukiwa umekakaa katika mitindo mbalimbali na laptop juu ya mapaja na." Hivo wanashauri laptop ikae juu ya meza wakati unafanya kazi zako

3.Utumiaji wa madawa ya kulevya watu wanaotumia madawa ya kulevya kama vile cocaine heroin,, methamphetamine, indian hep nk, hizi dawa zinaharibu sperms na hivyo basi kuathiri uwezo wako wa kuzaa

4.Ulevi wa kupindukia(alcoholism)-utafiti unaonesha kuwa unywaji wa kupindikia(walevi) wana kiwango kidogo cha uzalishaji wa manii na homoni za kiume yaani testesterone

5. Uzito wa mwili pia huathiri afya manii, wanasema wataalam. Ashiru anasema kudumisha uzito wa mwili husaidia kuweka mbegu za kizazi(manii) katika hali nzuri, kuwa overweight(uzito mkubwa) huweza kupunguza ubora wa manii na wingi.

Aidha, utafiti wa mwaka 2009 na Shirika la Afya Duniani wanaeleza kwamba,wanaume wenye uzito mkubwa-obese wana upungufu wa kazi za korodani(reduced testicular functions) hivo basi wanazalisha idadi ndogo ya manii

6. Mazingira ya kazi huathiri afya ya manii, tunaambiwa. Ashiru anaonya kwamba kufanya kazi katika mazingira ya moto, kama vile viwanda vya kuoka mikate(bakery) au Foundry pamoja na staili ya ukaaji muda mrefu ambao huongeza joto la korodani Hii inaweza kuathiri uwezo wa manii ya kukomaa,na kuzalishwa chache "profesa wa anatomy anashauri

7.Uangaliaji wa televisheni(TV) wa kupindukia ,Katika utafiti uliochapishwa katika Journal British of Sports Medicine, watafiti katika shule ya afya ya umma( Harvard School of public health-HSPH)umeonya kuwa vijana ambao wanakaa tu kutwa mzima kuangalia tv wanazalisha idadi ndogo ya manii kuliko wale ambao wanajishighulisha

Profesa utafiti / msaidizi mwandamizi wa lishe na magonjwa katika HSPH, Dk Jorge Chavarro, anasema "watu ambao waliangalia Tv kwa zaidi ya masaa 20 kwa wiki walikuwa na kiwango cha chini cha uzalishaji wa manii kwa asilimia 44% ukilinganisha na wale ambao hawakuangalia kabisa tv.
 
sasa hapo kwenye kuangalia tv kwa muda mrefu si ni mtihani kwa sie wengi wetu? Maana mie ni movie addict kila jioni inavyofika
 
Pia vichwa vya popo vinachangia... source mzizimkavu!!.....
 
sasa hapo kwenye kuangalia tv kwa muda mrefu si ni mtihani kwa sie wengi wetu? Maana mie ni movie addict kila jioni inavyofika

Calculate masaa unayoangalia

Sent from my BlackBerry 9300using JamiiForums
 
Na wenye kuwahi kufika kileleni je inahusika????
 
Punyeto vp?

Ha ha unfortunately haijatajwa sema punyeto ikizidi sana ina athari ya kulegeza musles(misuli) ya uume

Sent from my BlackBerry 9300 using JamiiForums
 
Na wenye kuwahi kufika kileleni je inahusika????

Kama mada ilivyo we talk about sperm count and quality

Sent from my BlackBerry 9300 using JamiiForums
 
kwani standard watching hours ni masaa mangapi??? naomba ufafanuzi kidogo juu ya hili am damn serious

Hemb piga mahesabu,umeambiwa ukiangala over 20 hrs una abt 44% low sperm count

Sent from my BlackBerry 9300 using JamiiForums
 
Back
Top Bottom