Hizi ndzio sababuziliso fanya serikali ifiche taarifa ya tume ya matokeo mabaya F4 2010

Qualifier

JF-Expert Member
Joined
Dec 14, 2012
Posts
1,252
Reaction score
405
Ndugu zangu wana Jf wote , mimi nimepitai taarifa ya tume iliyo undwa na waziri Mkuu kuchunguza matokeo mabaya ya mitihani ya taifa ya kidato cha nne mwaka 2010,ambayo serikali imeamua kuificha na kuunda tume nyingine 2013 kwa lengo la kuwa laghai watanzani wakati serikali inayo majibu yaliyo tolewa na tume ya 2010. Baadhi ya maoni yaliyotolewa na wadau yanaonyesha moja kwa moja udhaifu wa serikali unavyo changia kuporomoka kwa kiwango cha Elimu Tanzania. baaddhi ya hoja hizo ni hizi hapa:
1. Maaamuzi ya kitaalamu kuhusu uendeshaji wa Elimu hufanyika kisiasa bila kuzingatia utaalamu na utafiti.(ukurasa wa 7)
2. 1.5% tu ya walimu ndio waliopewa mafunzo ya matumizi ya mitaala mipya baada ya kubadilisha mitaala mwaka 2005
(uk.7)
3. somo la Mathematics linaupungufu wa walimu kwa 60.6% (uk.8(
4.upunguf wa miundo mbinu :
-Maabara za Chemistry pungufu 79.6%
-Maabara za Biology pungufu 66%
-Maabara za Phyiscs pungufu 65%
-Nyumba za walimu pungufu 72% (uk 9)
5. Baadhi ya watendaji huwadai rushwa ya ngono walimu wa kike ili wapangwe vituo vyenye mazingira mazuri ya kazi ndi maana walimu wa kike wanarundikana mijini wakati wakiume wanalundikana vijijini (uk 76)
kwa taarifa hii inayo onyesha mafanikio ya serikali ni 1.5% kutoa mafunzo kwa walimu juu ya matumizi mitaala na pungufu kwa 72% nyumba za walimu HEBU LINGANI mafanikio 1.5% kushindwa 72% itakuwaje wanafunzi wafaulu?
 
Mbona umefupisha sana? Nimelazimisha kasa yangu kumbe ni mwisho hapa!!

Sent from my BlackBerry 8520 using JamiiForums
 
Nitakutumia attachment usome taarifa nzima
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…