1.Usalama.
Kuzuia vitu vinavyohusiana na ujenzi, vikidondoka viwe eneo moja visiumize watu wa chini na wapita njia.
2.kuzuia uoga (phobia)
Kila binadamu ana uwezo wake wa kuhandle vitu, mfano kadri jengo linavyozidi kuwa refu, mwingine huweza kupata kuzunguzungu akiwa umbali wa floor fulani hivyo akiwa ndani ya uzio wa net inasaidia kumpa uwezo wa kujiamini na kufanya shughuli zake vizuri
3.Kuongeza umakini
Inasaidia kudeal na kazi zako husika kuliko kuangalia vitu visivyokuhusu nje hasa ukizingatia mtu upo juu zaidi.
4.Kuficha ujuzi.
Kila kazi Zina utaalamu wake, hivyo si vyema mtu kucopy na kupaste mambo, mfano: ramani, michoro, shepu ni design za mijengo mbalimbali bila ruhusa.
Siyo mtu anazoom jengo lako na kwenda kufanya habari zake kiholela.
5.Heshima na ustaarabu.
Jengo linaweza kujengwa uswazi /uswahilini, ambako nyumba nyingi ni duni huku vyoo na mabafu vikiwa ni vya nje tena havijafunikwa chochote juu. hivyo net husaidia watu wengine kufanya mambo yao kwa uhuru.
Yapo mengi ya kitaalamu zaidi , ila kamata hizi nyepesi nyepesi