Hizi ni salamu zangu za Pole kwa Wanawake wote mnaopitia Changamoto ya Uzazi

Hizi ni salamu zangu za Pole kwa Wanawake wote mnaopitia Changamoto ya Uzazi

Lethergo

JF-Expert Member
Joined
Aug 7, 2023
Posts
6,534
Reaction score
11,421
Wakuu.

Leo ngoja nije niwape pole mama zetu, dada zetu na wadogo zetu wa kike wanaopitia changamoto za uzazi.

Hauwezi amini ila amini amini nakuambieni maumivu ya mwanamke ya kuishi bila kua na mtoto wa kumzaa hayazungumziki na hayachunguziki.

Poleni sana wanawake wote mnaopitia changamoto za uzazi.

Hauwezi amini wakati wewe hautaki kuzaa kisa tu kwa sababu fulani fulani za kipuuzi ukishika mimba tu wewe huyooo unawahi kule kwenye mikasi na vizu vingi unaenda unatoa mimba kwamba Baba atanionaje au mama atanionaje nikibakia na hii mimba.

Usisahau kuna mwenzio hio mimba unayoitoa wewe yeye yupo anaitafuta kwa kila jinsi kila mbinu na kila namna ila wapi bila mafanikio mimba haiingii, mimba haikai, mimba inatoka yenyewe na hapati mtoto.

Poleni sana wanawake wote msio na watoto ila mnatamani mngekua na watoto wenu wa kuwazaa.

Nina imani ipo siku isiyo na jina Mungu atatenda na nyinyi mtaitwa "Mama".

Na nyinyi watoaji mimba Mungu awapeni mnachostahiri yaani msipate mimba milele mpaka mtubu madhambi yenu ya kuua vichanga na kudhulumu uhai.

Yangu ni hayo tu.
Niishie hapa.
I Lethergo yesterday!
 
Uko sahihi, wengine ni Maradh tu ila wengine ni kuutumia vibaya ujana, kumeza dawa za kuzuiya mimba, kutoa mimba n.k

Kuna jamaa alimtoa mimba kadhaa mdada mmoja kisha baada ya ndoa dada uzazi ukagoma, jamaa kaoa mwengine ila uzuri huyu hajamuacha, but it is painful.
 
Uko sahihi, wengine ni Maradh tu ila wengine ni kuutumia vibaya ujana, kumeza dawa za kuzuiya mimba, kutoa mimba n.k

Kuna jamaa alimtoa mimba kadhaa mdada mmoja kisha baada ya ndoa dada uzazi ukagoma, jamaa kaoa mwengine ila uzuri huyu hajamuacha, but it is painful.
Ndio mkuu wengine ni maradhi kweli hii nimeshuhudia lakini wengine pia ni maumbile yanachangia hii pia nimeshuhudia, nawapa pole wote wenye changamoto km hizo
 
Poleni sana na ambao bado mpo kwenye umri wa kupata mtoto Mwenyezi Mungu awajaalie

NB: nilikutana na mama mmoja mtu mzima akaniambia sikubahatika kupata watoto, ninyi ndo watoto wangu nili feel pain kwakweli! Inaumiza sana

Ukiwa kwake hasa jion anakuwa mtulivu sana, ama mpweke aseeh watoto ni furaha, amani na kila kitu!
 
Back
Top Bottom