Hizi seat covers za Safari Automotive ni next level

hawa jamaa wao vizuri sana ila sasa bei zao sio rafiki sana kwa tunaomiliki vigari vya bei nafuu na ukitaka kuhakkisha we angalia yale mandinga wanayoyafanyia kazi, ni gari za pesa kwenda mbele

kwa anaejua fundi mzuri wa seat covers kwa aARUSHA naomba msaada
 
hawa jamaa hawana customer care kabisa niliwahi kuwatembelea walivyonipokea tu nikabadili uamuzi wangu wa kubadili roof ya gari. Ila wanafanya vizuri ila customer care siyo nzuri kabisa.
kwenye hili naomba nikuunge mkono ni kweli hawana ukarimu kwa mteja... nilitaka kufanya nao kazi nikahairisha.
 
Safari wako Njiro Nanenane (nmesahau jina la kituo) na
Kuna fundi mwingine pale jirani na hospitali ya Seliani kama unaenda stendi ndogo.
 
Bei ya kukomoana (si rafiki kwa 'WANYONGE') Nilienda na Nissan Patrol wanataka 1.5m nikatafuta fundi mitaa ya Mabibo akanishonea kwa 450,000
Duu! Na zimetoka vizuri kabisa mpaka mwenyewe ukaridhika nazo?
 
kwenye hili naomba nikuunge mkono ni kweli hawana ukarimu kwa mteja... nilitaka kufanya nao kazi nikahairisha.
Ilikuwa mkoa gani? Hapo ndio biashara nyingi huwa zinakwama. Baada ya kupata mafanikio, wanaanza kuzingua.
 
hawa jamaa hawana customer care kabisa niliwahi kuwatembelea walivyonipokea tu nikabadili uamuzi wangu wa kubadili roof ya gari. Ila wanafanya vizuri ila customer care siyo nzuri kabisa.
Pole sana kwa yaliyokukuta nia Na dhumuni la SAFARI Automotive siku zote ni kukupa huduma Bora Na kazi yenye Ubunifu mkubwa sana.

tunamshukuru Mungu sana watanzania wametupa support kubwa sana - Na ata nilipoambiwa nije huku kuangalia maoni yenu Na kujibu nilikimbia faster kwasababu kwetu kila mtu ni mteja (nani asiyependa magari)????

UHALISIA - kwenye bihashara tumehudumia watu wengi sana Na ukweli huwezi kuwatosheleza mamia wote kuna mahali kama binadamau utakosea Na pengine ukahukumiwa kwa kosa hilo Na mema yote kisahaulika.

pale tunapokosea tunaambiwa tunafurahi kwasababu hapo hapo ndipo kuna mafunzo yetu Bora yakutupeleka hatua mia mbele.

kwa niaba ya uongozi wa safari automotive tusamehe Na vilevile kama kuna lolote twaweza fanya usisite kutupigia simu 0754757431

mama Karibu ofisini kabisa milango yote IMO wazi.

SAFARI Automotive spokesperson
 
Hiyo Seatcovers ni ya @safari_automotive

custom made Mteja anavyotaka taste yake Na tamanio lake
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…