NIONANAVYO, hapo pana vitu tofauti..kuna sheria za makosa ya jinai na sheria za madai, sheria za jina ni ugomvi kati ya mtuhumiwa na dola na aliyefanyiwa kitendo cha jinai i.e kuibiwa,anakuawa ni mlalamikaji tu i.e, shahidi kwa upande wa dola au jamhuri...katika kesi za madai..ni ugomvi,kwa lugha ya kawaida, kati ya mtu na mtu,yaani mdai na mdaiwa. Kesi za hapo juu ni kesi za jinai...ambazo dola kupitia,mkurugenzi wa mashitaka ndio wanaoziendesha na mahakama hutoa adhabu kwa mujibu wa sheria husika na kosa lenyewe.
Vipi mlalamikaji anapata haki yake katika jinai.
Inawezekana mfano katika hukumu kama hiyo hakimu au jaji,baada ya kutoa hukumu ya kifungo,kulingana na kosa linalohitaji hukumu ya kifungo,akamtoza faini mtiwa hatiani au fidia..mfano kesi ya ubakaji...kama ya babu seya...kifungo na fidia...ni uamuzi wa mahakama itakavyoona inafaa kwa mujibu wa kesi na mazingira yake...mara nyingi hutokezea katika kesi za uharibifu na upotevu wa mali kwa hujuma kama wizi.
Upande wa pili, mlalamikaji anaweza kufungua kesi ya madai...kudai fidia au kurejeshewa mali yake iliyopotezwa na mtuhumiwa katika jinai na kama hukumu imetoka anachofanya ni kuchukuwa kopi ya hukumu na mwenendo wa kesi katika jinai,ambayo haijakatiwa rufani au kuombwa kupitiwa na mahakama ya juu,na kuwa ushahidi wa kutosha kusukuma madai yake ya fidia i.e.,conclusive evidence
Kadhalika,bado mahakama inatoa nafasi baada ya hukumu kama za hapo juu ya pande husika kukata rufani kama hawajaridhika na kutiwa hatiani kwa mshitakiwa au kuadhibiwa kwake.