Shark
JF-Expert Member
- Jan 25, 2010
- 29,775
- 29,746
Wakuu Kwema?
Kuna Takwimu zimetolewa na TFF zikionyesha mambo mbalimbali yaliyotokea msimu ulioisha ikiwemo Timu iliyoingiza mapato mengi, Uwanja Ulioingiza Mashabiki Wengi, Timu yenye Mashabiki Wengi, etc.
Binafsi naweza nisiamini sana juu ya Mapato Kwa kila Uwanja au Mapato Kwa Kila Timu sababu ya upigaji, lakin takwimu hizi zinaweza kua kweli pia sababu ni kiasi cha kujua tu tickets zilizouzwa na mgao wa kila timu.
Shida yangu ni Takwimu za timu yenye Mashabiki Wengi, hapa "tumepigwa" mchana kweupe. Tunapokata tickets hua hatuandikishi sisi ni mashabiki wa timu gani, na isitoshe Mechi kama za Simba v/s Yanga ambazo zote ziko Dar dhana ya timu mwenyeji hua iko kwenye makaratasi tu, lakini kiuhalisia timu zote hua ni wenyeji.
Kama mechi ambayo Yanga atahesabika kua mwenyeji basi anapewa mashabiki wote sio sahihi maana hakuna takwimu rasmi za idadi ya mashabiki kwa kila timu kwenye mechi husika.
Yaani Inawezekana kwenye Mechi ya Yanga vs Simba idadi ya mashabiki wa Simba walikua wengi kuliko wa Yanga lakin sababu mechi hiyo Yanga walikua wenyeji basi mashabiki wote anapewa Yanga.
Ieleweke hapa sizungumzii kishabiki, bali aina ya takwimu na jinsi ilivyopatikana. Kama kuna hoja zaidi katika hili karibuni.