Uchaguzi 2020 Hizi teuzi na tengua ninazoweza ziita kuwa ni za "vurugu mechi" za Rais Magufuli zinaipeleka wapi nchi yetu?

Nchi ipo palepale Longitudes na Latitudes, kama wateule watakua kwenye kutafuta uongozi mwingine majukumu ya kiofisi atafanya nani
 
DC,RC DAS NA DED hao kusema kweli huwez kusema ni watumishi wa umma moja kwa moja...labda kidogo DED na DAS...Tuseme tu Rais ana mamlaka nao akiamka leo anaamua nini juu yao..
Tuseme wakuu wa wilaya leo wote waamue kwenda kugombea ubunge s atatengua wote na kuteua wapya ambao wanafika 123 ...n suala la busara tu acha wakagombee wakipita kura za maoni ndo unaweza kusema uteue wengine..
Ni kuongeza gharama zisizokuwa na tija ..kwenye sheria busara hutumika kwanza kukiko kuchukua hatua.
 
Mshika mawili lazima moja likuponyoke
Watu mnalalamika hakuna ajira,walio na ajira wanalalamika hawapandi vyeo
Hii ni safi nenda kagombee ili wengine wapate ajira,wengine wapande vyeo
ila wanaoteuliwa wana kazi tayari.
 
DAS na DED na RAS ni watumishi wa umma, hilo halina mjadala. DC na RC wanaitwa watumishi wa Serikali, kiongozi ajaye asipowataka wanakuwa wamepoteza ajira zao tofauti na DAS na DED hao wanaweza pelekwa sehemu nyingine
 
Sawa, lakini hiyo likizo bila malipo haina muda maalumu. Ni likizo tu haioneshi ni ya miezi mingapi kiasi cha kufanya nafasi iliyoachwa wazi isikahimiwe hadi likizo itakapoisha?
Kama hawajajiuzulu au kuacha kazi maana yake wataendelea kulipwa mishahara yao kama hawatateuliwa kwenye nafasi walizoomba, sasa huoni ni kuongeza gharama kwa serikali kulipa watumishi hao?
 
Hawalipwi, mbona nimeeleza hapo mkuu
 
Je kikatiba bado rais ana mamlaka ya kuteua?
Anayo mpaka siku anaapishwa raisi mwingine baada ya uchaguzi. Issue hapa ni kwanba hao watia nia hawajajiuzulu au kuacha kazi. Wanakuwa wameomba likizo bila malipo.
Na wasipoteuliwa kwenye nafasi walizoomba wanarudi. Wakiteuliwa basi ndiyo mwisho wa utumishi wao kwenye nafasi walizokuwa nazo.
 
Hizi teua na tengua zinazoendelea ktk kipindi hiki, zinatuthibitishia jambo moja na la msingi sana. Nalo si jingine bali kufanya kazi ktk mazingira magumu, yenye lawama nyingi sana na hata kukosa uhakika wa usalama ndani ya ajira zao ktk siku zijazo. Hii ni kutokana na Mkuu ataamkaje ama ataambiwa nini juu ya utendaji wako.

Katika awamu hii ya tano, miongoni mwa mihimili mitatu ya utawala wa nchi, huu wa serikali ambao wenye dhamana ya utekelezaji wa sheria na katiba, inadhihirisha unawalizimiu watendaji wa chini kufanya kazi kwa "pressure" kubwa mno. Ni wazi kuwa ktk mazingira hayo ajira hii haiuwavutii tena, hasa pale wanapokuwa kama "interface' ktk kusimamia utekelezaji wa majukumu yao na kukabiliana moja kwa moja kwa wananchi.

Tunapoona wengi wa wateule hao wakikimbilia kusaka ajira ktk mhimili wa bunge. Inatudhirishia kitu kimoja kuwa, wanaona ni vyema kuwajibika ktk kusema kuliko kutenda kwa vitendo. Kwa kuwa kwa kutenda kwa vitendo itawapasa pengine kuja kuwajibika kwa kuwa hawana kinga yoyote ile ya kutokushtakiwa. Bali kwa kuropoka tu bungeni na kuunga mkono hoja hata zile za kipuuzi hukutawanya kuwa na "any sanction" ktk siku zijazo.

Kwa hiyo basi, ajira ndani ya mhimili wenye mamlaka ya kutunga sheria, kuisimamia na kuishauri serikali ndiyo uliyo salama kwao. Mkulu ndiyo huyooo anajiandaa kwenda ktk orodha ya maraisi wastaafu. Thus, they real doubt what will be their aftermaths.
 
Kikatiba ya nchi hana...........

Ila kwa kuwa nchi yetu hivi sasa inaendeshwa kama gari bovu na Jiwe anapenda "kujimwambafai" ndiyo ameamua kutupeleka kukote kule anakotaka yeye!
unaweza ku quote fungu lipi la katiba
 

Mkuu ni vizuri ukajiuliza kwanza kuwa kwanini safari hii watia nia wengi ndani ya CCM ni wale wateule? ni wale akina "Ndiyo mzee? ni wale ma MC wapambaji wa sherehe majukwaani? kwanini wasitoke ktk muhimili wa Mahakama au Polisi etc//
 
Asante tunaye rais asiyekuwa na kanuni za utendaji. Ni hatari sana.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…