Hizo MW 5,000 unazozipigia chapuo Waziri Makamba zipo?

Hizo MW 5,000 unazozipigia chapuo Waziri Makamba zipo?

Hismastersvoice

JF-Expert Member
Joined
Jan 26, 2013
Posts
21,741
Reaction score
26,735
Watanzania tuna tatizo kubwa sana la upatikanaji wa maji safi na salama lakini serikali haifanyi juhudi kubwa kulitatua tatizo, huko Manyara, Arusha na Kilimanjaro wananchi wanatumia maji yenye kemikali hatari kwa maisha yao lakini Serikali inaona ni sawa tu, shukurani ziifikie Japani kwa kuahidi kusaidia mtambo wa kuondoa kemikali japo ni kwa eneo dogo lakini asanteni.

Hawa wanaokusanya kura huko hilo tatizo haliwahusu ndiyo sababu wanakimbilia kusiko na tatizo ila huenda kuna maslahi! Pamoja na kupata uhuru mwaka 1961 mpaka leo asilimia kubwa ya wakazi wa Dar wanajitegemea maji kutoka visima walivyovichimba, maji ya visima ambavyo yamechanganyika na maji taka na haviwekwi dawa. Katika hali ya kawaida serikali ingeanza na kujali afya za watanzania ili waje kuwa wazalishaji wazuri wa chakula na bidhaa.

Mhe. Makamba unapotuambia kuhusu MW 5,000 sisi wala hatuelewi kwa baadhi yetu umeme upo kwenye nyumba tuishizo ila kuutumia ni mpaka tuparurane ili hela ya kuununua ipatikane, maji tunategemea kisima cha Mpemba na mvua wakati wa masika, haya maji ya Mpemba mheshimiwa hauwezi kuyanywa na ukiyamwagilia kwenye bustani yako ya maua huenda yakafa kutokana na chumvi iliyomo sisi tunayaona matamu.

Tukiacha haya maji ya visima kama unskumbuka mwaka uliposafiri na gari toka Chalinze kuelekea Segera utakuwa uliwaona wanawake wakichota maji yanayofanana na chai ya maziwa kando ya barabara, maji hayo ndiyo wanakwenda kupikia, kuoga, kifulia na kunywa! Hawa hizo MW 5,000 wala hawataki kuzisikia japo nyie mnaziita ni za kimkakati!
 
Kwahiyo hutaki umeme unataka maji atakuja mwingine anataka kingine
 
Uandishi wa aya kwenye essay ilikuwa ni kwaajili ya kufaulu mitihani? Au ndo uanasayansi?

Hujui wapi anaanza zungumzia nini, mara paap, MW 5,000 kutokea kwenye tatizo la kutokuwa na maji.
 
Msio wahi kusafiri kwenda mikoani ninapozungumzia sizungumzii yakuoshea gari, wenzenu huko kaskazini mikoa ya Arusha na jirani watu wsmepinda miguu na meno yameharibika kutokana na kutopata maji safi na salama, fikiria familia nzima mnakuwa vilema sababu ya maji ambayo si salama, hawa wanaishi maisha ya shida isiyo kubalika nyie mnakuja na ujuaji.
 
Back
Top Bottom