Hizo ndizo gharama timu inaingia, pindi inapomsajili mchezaji toka nje

Hizo ndizo gharama timu inaingia, pindi inapomsajili mchezaji toka nje

sembo

JF-Expert Member
Joined
May 25, 2011
Posts
4,350
Reaction score
3,451
Pamoja na TFF kuongeza idadi za wachezaji wa kigeni [pro] hadi kufikia saba, kwa gharama hizi ni timu chache sana zinazoweza mudu hiyo idadi.

1. Ada ya kukuza Soka la Vijana.

Kila timu kuanzia sasa inatakiwa kulipga dola 2000 kwa kila pro ili kukuza soka la vijana. Sasa kama timu inao 7, itatakiwa kulipa dola 14.000 ambazo ni zaidi ya Tsh. 32.000.000.

2. Kodi ya Mapato.
Kuanzia msimu huu TRA inaanza kufanya yao katka ada za usajili na mishahara ya pro ambayo ni 18.5% ya kila watakachopokea. Kwa akili ya kawaida tu, kina Okwi, Niyonzima, Kipre na Twite hawatakubali mpunga waliozoea kupokea kupungua hivyo mzigo wote utaenda kwa timu.

3. Kibali Cha Kufanya Kazi Nchini.

Immigration humpa Pro yoyote anayekuja kufanya kazi nchini kibali ada yake ni dola 600 kwa miaka 2. Sasa imagine timu ina pro 7 kocha 2, jumla yao 9 ambapo gharama zao ni dola 5,400 ambazo ni zaidi ya Tsh. 12,420,000 na gharama hizi hulipwa na timu.

My Take:
"Survival of the fittest" ndo mda wake kuchukua nafasi.
 
Safi sana...
Timu zigeukie vijana sasa...
 
Kwa hyo mkuu unaona ni bora niyonzima kuchukua dola 3000 =TSH 6,500,000 kwa mwezi bila kukatwa kodi huku daktari anayelipwa tsh 1,200,000 kwa mwezi akikatwa takriban sh 250,000 kwa mwezi??? kwangu mm naona huu uamuzi umechelewa sana. kama mzigo wa kodi utahamia kwn timu ni uzembe na usanii wa viongozi wa vilabu kufanya madili yao kugawana na wachezaj mishahara.
 
Hapana Mkuu.. lengo langu lilikua ni kuonesha hizi gharama mpya katka timu zetu.. Kama Yaya Toure anapokea paund 250,000 kwa wiki, lakini take home yake ni paund 165,000.. kwanini isiwe kwa kina Haruna na Okwi?

TRA wana haki ya kukusanya chao.. Na waanze hili zoezi haraka.. kama noma na iwe noma.
 
Hao TRA wamechelewa sana kukata kodi kwa wachezaji.!
 
Nategemea kumuona Mh. Jamal Malinzi akiitisha mkutano Tansoma Hotel.. akijitapa kua katika uongozi wake ameongeza mapato ya serikali kupitia wachezaji kukatwa kodi.
 
Kwa nini TFF inatoza kwa dola? Serikali hawalioni hili?
 
umefika wakati hata mkulu naye akatwe kodi jamani,kwa nini yeye hakatwi??
 
Back
Top Bottom