WomanOfSubstance
JF-Expert Member
- May 30, 2008
- 5,457
- 963
Inakuwaje mbunge ulalamike ati kuna watu wananyemelea jimbo lako! Kwani hilo jimbo umeliwekea "hatimiliki"? Nijuavyo mimi mtu anapopata ubunge, anadumu miaka mitano kisha uchaguzi unapowadia wananchi watapima na kuamua wamrudishe au wamuondoshe ili waweke mtu mwingine atakayewahudumia vema.Sasa wananchi watachagua vipi kama incumbent anang'ang'ania na kukataa ushindani? Nimeshaona hadi sasa wabunge kadhaa "wakilia" wanaingiliwa majimbo yao - mfano ni mama Anne Kilango Same Mashariki na Dr Zainab Gama - mbunge wa Kibaha.Badala ya kulialia kwanini msiache wananchi ( mabosi wenu) waamue wanamtaka nani?
Ndugu yangu kama mpiga kura je hii imekaaaje?..kwangu mimi imekaa vibaya sana!
Ndugu yangu kama mpiga kura je hii imekaaaje?..kwangu mimi imekaa vibaya sana!