Hodi hapa

Mokoyo

JF-Expert Member
Joined
Mar 2, 2010
Posts
15,145
Reaction score
5,566
Hodi hapa, nimekuwa mgeni kwa miaka miwili sasa na leo nimeamua kuingia humu ndani. Nimesoma maandiko mengi sana ya kila idara nami nimeingia kuchangia.





Misimamo yangu ni kama ifuatavyo
  • Nahitaji heshima kama ambavyo nitakuwa naitoa
  • Sipendi malumbano yasiyokuwa na tija ni vyema kujenga hoja zenye maana na mashiko
  • Huu ni mtandao na kwa mtu mwenye akili timamu anajua maana ya mitandao na varieties za watu walioko katika mitandao hapa hakuna cha urafiki wala undugu, kazi ni moja tu kuchangia mada, nafikiri nimeeleweka
Kuna wanaouliza mantiki/hoja ya andiko langu, iko wazi kama hujafumba macho na inaeleweka kuwa JF ni kioo cha jamii lakini kumekuwa na ukiritimba wa kupeana yasiyotakiwa kutokana na kusujudiana kusikotakiwa baina ya binadamu.

Hoja yangu ni hii kuwa hata mnyama hapendi anaposingiziwa tabia za kihuni na kipumbavu za binadamu, manthalani kubaka, anapobaka mtu mwenye akili timamu watu wanasema amefanya kitendo cha kinyama, si kweli hata kidogo ni kuficha udhaifu wa binadamu kwenye mhimili wa wanyama ambao wana haki zao. Hili linaingia moja kwa moja hapa JF kuna watu wamekosa pa kufanyia ufirauni wao wamekuja hapa JF kumbuka akisemacho na kukiandika mtu ndio kimeujaza moyo wake.

Kilio ni kilio haijalishi kinatoka kwa nani kinachoweka tofauti ya kilio ni suala lililo sababisha kilio. Nasema hivi kwasababu kuna kilio cha kufiwa na ndugu au rafiki hivi viko tofauti lakini vilevile kuna kilio kwasababu ya kufukuzwa kazi nacho hiki kiko tofauti. Pia msisahau kuwa kuna kilio kwasababu ya kukimbiwa au kuachwa na mpenzi, mume au mke navyo hivi ni vilio na machungu yake anayajua yeye aliae.
Maana yake ni kwamba kila mtu ana jukumu na wajibu wake kuhakikisha kuwa kuna tofauti ya kuwa JF na kuwa pengine popote pale na kinachofanyika hapa ni kusaidia tu upunguze makali ya majonzi yako lakini sio kuondoa majonzi yako.

Kwa wenye fikra pevu wamenielewa kwa wenye mtindio wa ubongo ndio watakuja na maswali hoja iko wapi sasa hapa, umeingia kwa mbwembwe pamoja na kutaka kujua jinsia yangu, nani alikuambia nimekuja JF kutafuta mke au mume. Niko hapa kubadlishana uzoefu wa kimaisha na kuelekezana kuondoka katika mawaa na kwenda katika mistari minyofu.
 
kwa hiyo bwana/bi Pazia, hapo juu hoja ni nini?
 
umeshapata senksi moja tayari au ndio nimekuuzi tayari. mbona unaingia na mikwara hevi.
 

Ahsante kwa kuwa mwanachama,ahsante kwa kujiunga,ahsante kwa kuchangia,ahsante kwa posts,ahsante sana Pazia.Ahsante najua utatutajia jinsia pamoja na status yako.Ahsante kukaribia jamvini.Oh!..........!!!
 
umekuja kwa mbwembwe mno...
slow down tafadhali...
hatukupi thanx hivi hivi...
tunatoa thanx kama unaloongea la maana.
 
Duuuuuuuuu......... ama kweli we pazia............maana naona unafuta upepo wa baadhi ya watu humu ndani............... USIKARIBIE
 


Its more blessed to give than to receive!
 

where is Mwiba when we need him?
 
MMh Karibu!

Karibu Pazia; naweza kuhoji kwanini umechgua jina PAZIA ilhalia mchango wako haundani na sifa ya kufunika?

Eerrrrr .........ni katika kutaka kufahamu tu.
 
MMh Karibu!

Karibu Pazia; naweza kuhoji kwanini umechgua jina PAZIA ilhalia mchango wako haundani na sifa ya kufunika?

Eerrrrr .........ni katika kutaka kufahamu tu.
Kwani michango wangu imekaaje Mkuu?

Hili ndio jina langu halisi sio nickname
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…