Hodi hodi na msaada...

Hodi hodi na msaada...

Dr-of-three-Phd

JF-Expert Member
Joined
Oct 20, 2010
Posts
202
Reaction score
30
Nilikuwa naelekea mjini nikiendesha gari langu na nikagongwa ubavuni kushoto na gari la jamaa aliyetokea kwenye barabara ndogo akakimbia nikaweza kuchukua namba ya gari lake, nifanyeje nipate details za gari hilo ili niendelee na kesi?

Asante kwa msaada wenu

Mdau
 
Nenda TRA, wakiingiza hizo namba kwenye system watapata information zote. But unaweza kuta ni za pikipiki maana watu wetu wa IT kwa kuchanganya mambo ni hodari.
 
asanteni wadau, nitafanya hivyo, je TRA watanifanyia hivyo bila kuwa na report yoyote inayowalazimisha/amuru kisheria kufanya hivyo?
 
Nadhani busara ni kureport polisi kwanza kabla hatua zaidi hazijachukuliwa! Ila ni lazima ushahidi uwepo maana isiwe ni mtu una kisa naye ukaamua tu kumtafutia sababu!
 
Nadhani busara ni kureport polisi kwanza kabla hatua zaidi hazijachukuliwa! Ila ni lazima ushahidi uwepo maana isiwe ni mtu una kisa naye ukaamua tu kumtafutia sababu!

Dah! unawaza mbali sana mkuu...!
 
Asanteni wandugu na msaada huu wakunifanya nifikirie nje ya boksi zaidi.
 
Ni kweli cha kwanza polisi na ingekuwa vyema kuripoti wakati huo huo wa ajari na pia unamjulisha insurer wako kuhusu hilo ili yeye pia aweze kukulipa au kukutengenezea gari yako. Kwa kutumia maelekezo yako insurer wako anaruhusiwa kumshitaki huyo jamaa na kudai fidia (subbrogation). Utata wowote wa kuchelewa kuripoti huwa unaleta mashaka na unaweza usifaidike na chochote hata kama namba za huyo jamaa unazo.
 
Tatizo hapo atadhibitishaje kama kweli huyo jamaa alimgonga? Ana ushahidi wowote?
 
Back
Top Bottom