Hodi hodi Wana JF

Kamsweetie

Member
Joined
Oct 30, 2012
Posts
37
Reaction score
23
Nimefurahi kupata wasaa wakujitambulisha kwenu wana JF, kama lilivyo jina langu mimi ni kamsweetie mpaka tabia, nategema kujifunza mengi kutokana kwenu na vile vile kujuzana mambo muhimu katika jamii yetu!
Wapi mdumange wakukaribisha wageni jamani? Nani yuko kamati ya vinywaji na chakula? :bange:
 
Karibu sana jamvini, naitwa Katavi ni mlinzi wa jukwaa hili, unaletewa kinywaji na sweetlady, Globu atakuelekeza mitaa ya humu ndani na kukutambulisha kwa wenyeji.
 
Last edited by a moderator:
Karibu sana jamvini, naitwa Katavi ni mlinzi wa jukwaa hili, unaletewa kinywaji na sweetlady, Globu atakuelekeza mitaa ya humu ndani na kukutambulisha kwa wenyeji.

Haa ha ha Mkuu Katavi nipo kwa ajili ya kuwatembeza wageni. Karibu sana jamvini Kamsweetie angalia sana kuna vichochoro vingi mno, usije ukapotea.
 
Last edited by a moderator:
Ndugu zangu Katavi, Sweetlady (ulinizidishia kinywaji ndio maana sijaoneka kabisaaa jana) Globu (bado sijajua mitaa), Spike Lee, Ritz na Ulimakafu nawashukuruni sana kwa ukarimu wenu.
Siku njema
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…