LOGARITHM
JF-Expert Member
- May 5, 2010
- 974
- 475
Waheshimiwa Wana JF na wapenda maendeleo wote. Mimi ni mwanachama mupya kabisa nabisheni hodi. Nimeipenda hii forum na nimekuwa msomaji mzuri sana kwa muda mrefu. Sasa ni wakati wangu wa kujumuika kivitendo kama ilivyo wakati muafaka kwa ukombozi wa Tanzania yetu, kwa ajili yetu na vizazi vyetu vilivyopo na vijavyo. Naamini sawasawa na mawazo ya Balozi wa Ujerumani nchini kuwa Tanzania yenye neema kwa watu wake inawezekana mno ikiwa tu tutaweza kufanya mambo yaliyo sahihi.