Waheshimiwa Wana JF na wapenda maendeleo wote. Mimi ni mwanachama mupya kabisa nabisheni hodi. Nimeipenda hii forum na nimekuwa msomaji mzuri sana kwa muda mrefu. Sasa ni wakati wangu wa kujumuika kivitendo kama ilivyo wakati muafaka kwa ukombozi wa Tanzania yetu, kwa ajili yetu na vizazi vyetu vilivyopo na vijavyo. Naamini sawasawa na mawazo ya Balozi wa Ujerumani nchini kuwa Tanzania yenye neema kwa watu wake inawezekana mno ikiwa tu tutaweza kufanya mambo yaliyo sahihi.
Ndugu Katavi na wengine , nashukuru kwa ukaribisho wenu. Nimejiita jina hilo kwa kumbukumbu ya jinsi hesabu zilivyonishinda na zilivyonigaragaza enzi hizo. Lakini zile za kariakoo shimoni sio mbaya, hizo, naziweza!
Duuh, wewe kweli LOG zilikusumbua mpaka umesahau hata huwa zinafundishwa kidato kipi, hesabu za LOG huwa zinafundishwa form two baada ya kusoma quadratic equations, exponents na indices. Anyway, labda nyie mlikuwa mnafuata syllabus tofauti. Ni maoni tu!