Hodi hodi hatutaki,
Sisi tuko faraghani,
Tunakula mishikaki,
Mwaja sasa ni kwanini,
Wageni muwe pembeni.
Moyoni hatuna chuki,
Hilo liwe akilini,
Na hapa hatuondoki,
Hata pakiwa gizani,
Wageni muwe pembeni.
Hatutaki unafiki,
Mlikotoka rudini,
Mwajifanya marafiki,
Leo kwasababu gani,
Wageni muwe pembeni.