Salam twaitikia, huu ndio ufunguo,
Acha woga karibia,hapa ndipo kimbilio,
Usihofu nakwambia,hutopata kalipio,
Karibu ndugu karibu,uje pata matukio.
Asante JIDU pokea,kwa hofu kuniondoa,
Funguo nishapokea,na ndani nimeingia,
Roho imenitulia,mazuri nasubiria,
Kwahakika sitasita,maoni yangu kutoa.
Nimeanza pitapita,huku kule humu ndani,
Ya busara kutafuta,yafaayo maishani,
Mengi nimeshayapata,na hayana nuksani,
Kwahakika sitasita,maoni yangu kutoa.
Vyumba vingi nimeona,ila hiki chanivuta,
Kidogo nimesonona,wengi wanaokipita,
Najua wanakiona,ila lugha mewapita,
Kwahakika sitasita,maoni yangu kutoa.
JIDU na wewe GLOBU,hakika mmenivuta,
Kuwasifu ni wajibu,subira mmeivuta,
Acha nende taratibu,uzoefu kutafuta,
Kwahakika sitasita,maoni yangu kutoa.