Hofu imetanda Avic town

pwilo

JF-Expert Member
Joined
May 27, 2015
Posts
10,913
Reaction score
13,876
Ikiwa yamebaki masaa machache kuelekea mchezo wa Caf confederation cup utakaochezwa kesho jioni saa 10:00 Alasiri kati ya dar es Salam young African na club africain hali imekuwa tofauti kidogo kuanzia kwa mashabiki wake mpaka viongozi wake hofu imetanda pale avic town huku kila mmoja akisubiria nini kitatokea kwenye mtanange huo hakuna majigambo kama ilivyokuwa mechi ilyopita dhidi ya al hilal hali ilikuwa yenye kuleta matumaini kwa mashabiki na kila mtu alitamba kushinda mechi hyo tujikumbushe kidogo ilivyokuwa kauli za mechi iliyopita:–

Ali kamwe alitamba na kuwaaminisha mashabiki kwenye mechi iliyopota dhidi ya al hilal kwamba yanga ni kubwa kuliko al hilal na wamefanya investment kuliko wao na akawaahidi mashabiki al hilal anaenda kupigwa kama ngoma pale kwenye dimba la Benjamin mkapa kilichotokea kila mtu alishuhudia au kama alikuwa mbali alihadithiwa ila hali ni tofauti kwa mechi ya kesho kwani mpaka sasa hajatoa kauli yoyote kuelekea mchezo huo zaidi ya kuhamisha chanjo tu anaogopa yasije jirudia ya al hilal.

Mashabiki wao toka msimu huu uanze wa Caf champions league hawajaenda airport kuwapokea wageni wa wapinzani wao baada ya wao kupata kazi ya kufanya na walikuwa na matumaini ya kufika mbali baada ya kumpiga zalan fc kama ngoma ila al hilal wakakatisha ndoto zao na wao wamepoa huku wakiwa hawajui hatma yao kwenye mchezo wa kesho nao wapo kimya hakuna tambo wala majigambo wamejawa na hofu maana hawaijui kesho yao.

Haji manara huyu ndo anajiita mzee wa propaganda east Africa na Africa kwa ujumla alianza na THE RETURN OF THE CHAMPIONS ikadondokea pua akaja na IWE JUA IWE MVUA ikafa kifo cha mende mpaka sasa mzee wa propaganda hajatoa tamko lolote kuhusu mechi ya kesho maana hajui kitakachotokea ameamua kukaa kimya asije akaumbuka tena kama mechi zilizo pita ameshajua propaganda haichezi mpira ameamua bora akae kimya asubirie qudra za Allah tu kweli hofu imetanda.

Engineer hersi ni juzi tu hapa ametoka kusema mashabiki wa yanga wala mihogo hawana msaada wowote wala mchango kwenye team wanalalamika team ikifungwa na kuwataka waache tabia hyo kwani hata MAN CITY na PSG licha ya uwekezaji mkubwa ila hawaja pata mafanikio yoyote kwenye UEFA champions league huku akisahau soka la Africa na ulaya ni tofauti bora hata angetoa mfano team ya PYRAMIDS angeeleweka kuliko ulaya maana ni mbingu na ardhi.

Msimu uliopita engineer hersi na aliyekuwa msemaji wao ambaye amepigwa ban na TFF walionekana hadharani wamevaa jezi za team pinzani iliyokuja kucheza na mtani hawakuishia hapo walionekana kuwapokea viongozi hao wa team pinzani na kuongea nao kwenye simu ila msimu huu ni tofauti wamepoa sana hasa kuelekea mechi ya kesho hakuna hata anayesema Kesho wana piga mtu kama ngoma kila mtu amejawa na hofu kuelekea mchezo huo.

Wale kina aziz ki, gael bigirimana(former Newcastle player), dokta aucho, mzee wa kutetema, mdaka mishale, zanzibar finest, djuma shaaban, tuisila kisinda, faridi musa, jesus moloko, kesho ndio siku yao kuonyesha wao ni professional players and experienced players katika league ya NBC premier league na east Africa kwa ujumla huku kukamia mechi moja hakuna msaada wowote kwa team hamjawasili wale waje kucheza na ihefu au geita gold wale waliletwa kwa mashindano ya kimataifa na kesho ndio siku yao ya kuonyesha kwa nini dar es Salam young African iliwasajili alamsik.

NB: walijua rahisi kucheza Caf champions league sasa wanaionja pumzi ya moto huku mashabiki na wapenzi wa simba sports club wakiwaangalia wanavyotapatapa maana washazoea hizo mbilingembilinge.

Inah Allah maaswabirin wa man jitihada wajada.
 
Umevurugwa wewe sio bure, mechi acheze yanga mateso upate wewe kolowizard? 🚮🚮🚮
 
Umevurugwa wewe sio bure, mechi acheze yanga mateso upate wewe kolowizard? [emoji706][emoji706][emoji706]
Hivi wale mashabiki walio kuwa wanaenda airport kupokea wageni walikuwa wa team gani?
 
🤔🤔🤔🤔
 
Unafikiri kimataifa kuna shortcut kule? Hiyo njia ya machozi, jasho na damu lazima uipitie kama unataka kuwa mkubwa. Ulifikiri ukimrudisha reject kisinda, reject bigilimana, na kuwaleta kina aziz ki ndio itakuwa shortcut ya kucheza championsleague? Mna safari ndefu sana mpaka muwapigie simba magoti wawape mbinu, shwain topoloz
 
Bahasha ndio ziliwafikisha apa
 
Kile ni kikundi cha wahuni, hata mechi zao hawajui wanashinda vipi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…