Kama hakuwa na cheo tanu mchango wake kwenye kudai uhuru ni mdogo sana
Laki...
Kughitilafiana katika fikra ni silka yetu binadamu.
Mimi nimepata umaarufu mkubwa na tuzo kadhaa kwa kuandika kitabu cha Abdul Sykes.
Miaka 23 iliyopita niliandika kwenye shajara yangu taarifa kuwa Abdul Sykes na Julius Nyerere waligimbea nafasi ya urais wa TANU tarehe 17 April 1953 katika Ukumbi wa Arnautoglo.
Kisha nikaandika kutawazwa kwa Malkia Elizabeth II chini yake nikaandika tarehe ya uchaguzi wa Rais wa TAA mwaka 1953.
Uchaguzi ulifanyika Arnatouglo Hall tarehe 17 April 1953 kati ya Abdulwahid Kleist Sykes na Julius Kambarage Nyerere.
Wakati huu nilikuwa katika utafiti wa kitabu cha Abdul Sykes.
Taarifa hizi mbili katika Nyaraka za Sykes zilinisisimua sana.
Sababu yake ni kuwa ingawa Judith Listowel alikuwa ameeleza uchaguzi huu katika kitabu chake, "The Making of Tanganyika," (1965) hakueleza tarehe ya uchaguzi ule.
Jambo la pili ni kuwa baada ya uchaguzi huu uongozi mpya wa TAA President Julius Nyerere na Vice-President Abdul Sykes pamoja halmashauri yote ya TAA waliandika barua ya pongezi kwa Malkia Elizabeth na wote walitia saini zao katika barua hii.
Barua hii ipo katika Nyaraka za Sykes.
Mwaka wa 2012 Prof. Issa Shivji, Prof. Saida Othman Yahya na Dr. Ng'waza Kamata walipokuja kunihoji kuhusu historia ya Julius Nyerere wakati wanaandika "Nyerere Biography," (2020) waliniomba nakala na niliwapa.
Imekuwa kawaida kila nikiingia Maktaba kupumzika lazima nitakuta kitu.
Tutazame hizi Nyaraka za Sykes katika "In Praise of Ancestors," makala iliyozua taharuki.
Katika rejea kutoka Nyaraka za Sykes foot note no. 16 kuna barua ya Julius Nyerere ya tarehe 10 August, 1953 anamwandikia Gavana Edward Twining.
Kwa mara yangu ya kwanza kuiona saini ya Mwalimu Nyerere nje ya saini yake kwenye noti nimeiona kwenye hizi Nyaraka za Sykes.
Lakini nilikuwa nasisimkwa na mwili pamoja na akili pale Ally Sykes alipokuwa akinieleza mazingira yaliyopelekea kuandikwa kwa barua fulani.
Kitendawili nilichokutananacho kilikuwa rasimu ya katiba ya TANU.
Katiba hii iliyeyuka kama moshi.
Haipo kwenye Nyaraka za Sykes wala Maktaba ya CCM Dodoma.
Katika Maktaba ya CCM nilionyeshwa majalada mengi lakini karibuni yote kulikuwa na nyaraka zilizonyofolewa.
Nilibahatika kuliona jalada la Hamza Mwapachu na jalada la Abdul Sykes.
Majalada yote haya hayakuwa na hata karatasi moja ndani.
Nilipata tabu sana na mhariri wangu wa kitabu cha Abdul Sykes alipokuwa anaupitia mswada kwa ajili ya kuchapa kitabu.
Mimi nilikuwa nimeandika nyaraka zimeibiwa yeye akinitahadharisha kuhusu neno hilo la kuibiwa akiniambia linaweza kusababisha matatizo tukashitakiwa.