Hofu Kigamboni: Adaiwa kuua walinzi wawili na kujeruhi wengine kwa kuwagonga kwa Lori baada ya kushindwa kesi ya madai

Hofu Kigamboni: Adaiwa kuua walinzi wawili na kujeruhi wengine kwa kuwagonga kwa Lori baada ya kushindwa kesi ya madai

Mkalibari

JF-Expert Member
Joined
Mar 20, 2012
Posts
659
Reaction score
399
Habari Wadau ,hivi Sasa nimepitia maeneo ya Kigamboni Tungi kwenye Round about kuelekea Darajani,Kibada na Feri kwa mbele kidogo Kuna Kituo Cha mafuta.

Nimekuta Kuna zogo kubwa la watu,kutahamaki ni milio ya Risasi na watu wanakimbia hovyo.

Sijajua chanzo rasmi ni Nini,japo wengi wanasema kile Kituo Cha mafuta kina mgogoro wa umiliki.

Nimeona mabaunsa zaidi ya 10 wakizunguka zunguka wengine wameshika mapanga na wengine wameshika Bunduki.

Taharuki ni kubwa na istoshe watu ni wengi kwakua Leo ni siku ya mnada wa wakazi wa kikagamboni eneo lile.

Pia Kuna taarifa zisizo rasmi kua Kuna watu wamekufa kwa kukaganyagwa na Roli liloingia kwa Kasi ndani ya sheli na kuondoka Kasi pasipo kujulikana ni Nani alikua analiendesha.

Baadae niliona polisi wanaingia kutuliza ghasia,Mimi kwa usalama wangu nikaamua kuondoka zangu.

Sijui Kuna Nini siku hizi,michezo ya Bunduki imeanza Tena

Update
Yeah nasikia mabati Yale yamewekwa alfajiri ya leo kuzunguka eneo lote,na nembo na jina la sheli zikazibwa na stika baadae wakawekwa mabaunsa kibao kulinda hapo.

Ndio mida ya jioni imekuja kichwa Cha Roli kikiwa Kasi kigaingia ndani kwa kugonga mabati Yale na kikakanyaga watu kadhaa na inasemekena wamekufa papo hapo, hofu ni kubwa Sana aiseh.


---
JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
WIZARA YA MAMBO YA NDANI
JESHI LA POLISI TANZANIA


TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI​

Dar es Salaam 27, Agosti, 2021

KUKAMATWA KWA MTUHUMIWA WA MAUAJI YA WATU WAWILI WILAYA YA KIGAMBONI​

Jeshi la Polisi Kanda Maalim Dar es Salaam linamshikilia Mohamed Jumaa@Lardh JM (37),Mkazi wa Kariakoo kwa tuhuma za mauaji ya walinzi wawili waliofahamika kwa majina ya Eliakim Morali(30), Mkazi wa Mbezi Beach, Mlinzi wa Kampuni ya LOCK FORT SECURITY na Saunkoo Bakari(35), Mkazi wa Buguruni, Mlinzi Binafsi (BAUNSA).

Mnamo tarehe 26 Agosti, 2021 majira ya saa 12 jioni huko eneo la Tungi Wilaya Kigamboni katika kituo cha kuuzia mafuta cha JM PETROL STATION, mtuhumiwa aliwaua walinzi hao kwa kuwagonga kwa makusudi na gari lenye namba T 176 CVP aina ya DAF lori lililokuwa na tera ambalo halina namba za usajili.

Mtuhumiwa alifika katika kituo hicho cha kuuzia mafuta cha JM PETROL STATION alichokuwa ana kimiliki kwa ajili ya kuhamisha mali zake lakini alichukua gari lake na kutoka nje ya kituo na ghafla alirudi nalo kwa kasi huku likiwa halina tera na kuwagonga walinzi hao waliokuwa getini na kupelekea kufariki dunia papo hapo na kuwajeruhi watu sita ambao walikimbizwa hospitalini kwa matibabu.

Mtuhumiwa huyo alikuwa na kesi ya madai namba 118/2018 mahakama kuu iliyofunguliwa na ACCESS Benki baada ya kushindwa kulipa mkopo kwa muda muafaka aliochukua katika benki hiyo na mtuhumiwa alishindwa mahakamani licha ya kukata rufaa mara kadhaa na hatimaye mahakama ilitoa amri ya kuuzwa kwa kituo chake cha kuuzia mafuta maarufu kama JM PETROL STATION kilichopo kigamboni.

Jeshi la Polisi Kanda Maalum Dar es Salaam linaendelea na uchungunguzi wa kina juu ya tukio hili na mtuhumiwa atafikishwa mahakamani hivi karibuni kujibu tuhuma zinazomkabili.

Imetolewa na:-
MULIRO J.MULIRO- ACP
KAMANDA WA POLISI,
KANDA MAALUM,
DAR ES SALAAM

.
JamiiForums-2119681016.jpg

 
Asubuhi nilipita hapo niliona watu wengi sana na kituo kimezungushiwa mabati!
 
Asubuhi nilipita hapo niliona watu wengi sana na kituo kimezungushiwa mabati!
Yeah nasikia mabati Yale yamewekwa alfajiri ya leo kuzunguka eneo lote,na nemba na jina la sheli zikazibwa na stika baadae wakawekwa mabaunsa kibao kulinda hapo.

Ndio mida ya jioni imekuja kichwa Cha Roli kikiwa Kasi kigaingia ndani kwa kugonga mabati Yale na kikakanyaga watu kadhaa na inasemekena wamekufa papo hapo,hofu ni kubwa Sana aiseh....
 
Yeah nasikia mabati Yale yamewekwa alfajiri ya leo kuzunguka eneo lote,na nemba na jina la sheli zikazibwa na stika baadae wakawekwa mabaunsa kibao kulinda hapo...
Mabaunsa wameshindwa kuzuia kichwa roli?Sasa wanafuga hivyo vifua vyao Nini? Vifua Kama matako ya mtoto vile.
 
Wanaume wa Dar acheni uoga bana [emoji1787]
Hapo mzee lazima tuogope,maana Risasi zinarushwa hovyo Wala uwezi jua itatua wapi.

Wewe imagine Risasi zinapigwa alafu hapohapo Kuna mafuta ya petrol lazima uwe muoga.

Mf.kuna mmama naona walimchanganya na Nani sijui akiwa ktk gari yake ndogo yenye tinted Basi walimfukuzia wakafyatua Risasi hovyo,mpaka akaingiza gari mtaroni na akaizimia akawa hajitambui....
 
Hao wote wanaogombea hapo ni MATAGA family wanaoneshana umwamba.
Wacha washikane makalio,tutakuja kuwasuluhisha.
 
Back
Top Bottom