Uchumba ni ahadi ya kufunga ndoa siku za mbele. Ni kipindi cha kufahamiana kati ya wachumba kwa mema na makasoro aliyonayo mwenzake ili baadaye siku ya masiku waweze kufunga pingu za maisha. Na pete ya ucumba ni ishara wazi/ ya nje ya kuonesha na kumkumbusha mchumba kuwa ana mtu wake.
Kwa kuwa uchumba si ndoa bali ni ahadi ya ndoa sioni kwa nini Lusanji anasita kuidhinisha rasmi uchumba huo na kijana wake kwa kuivishana pete ya uchumba. Ikiwa mbeleni mambo yatashindikana basi itabidi wafuate mkondo tofauti.
Lakini naona faida ya kuidhinisha uchumba kwa sasa ni kubwa zaidi kuliko hasara. Kwa kuidhinisha uchumba na kuivishana pete daima popote watakapokuwa itawakumbusha kwamba wao ni "mali" ya mwingine. Kumbe hii inawaamshia uthabiti na nia imara ya kuhimili vishawishi kwa sababu kila mmoja atakuwa anakumbuka ahadi aliyo nayo kwa mwenzake, yaani kuwa mwaminifu na kujiheshimu. Umbali kati yao na kutoonana mara kwa mara kitakuwa kipimo kikubwa cha seriousness ya kila mmojawao.
Kumbe kama wanapendana kikweli, Lusanji asiogope. Na kama anamfahamu mwenzake vizuri hana sababu kubwa ya kutokumwamini. Japo mi ninavyoona hii stori inaonekana Lusanji ndo hajiamini, lakini kule kutokujiamini kwake anakutupia kwa mwenzake. Lusanji ndo mwenye matatizo. Bado yuko safarini, hajafika kwenye kituo cha moyo wake. Kwa lugha nyingine hajaridhika na ijana. Bado anatafuta kijana aliye bora zaidi kwa kipimo chake Lusanji. Atulie.