Hofu tunazaliwa nazo au tunazijifunza?

Hofu tunazaliwa nazo au tunazijifunza?

dgombusi

Senior Member
Joined
Sep 3, 2017
Posts
141
Reaction score
200
Je, unajua kuwa watoto hawazaliwi na hofu ya nyoka au buibui?

Wanafalsafa wa saikolojia wanasema kwamba binadamu huzaliwa na hofu mbili pekee: urefu (kuanguka) na kelele kubwa.

Hofu nyingine zote, ikiwemo ile ya wadudu, hujifunzwa polepole kadri muda unavyopita.

Watoto hujifunza kupitia udadisi kabla hofu haijaanza.

Utafiti wa American Psychological Association unaonyesha kuwa mwitikio wa hofu huathiriwa na uzoefu(Experience), utamaduni, na mazingira.

Ndiyo maana mtoto anaweza kucheka anapoona nyoka lakini akapigwa na butwaa akiwekwa juu ya sehemu ya juu—ubongo wa binadamu umeundwa kutambua kuanguka kama tishio la haraka!

Kwa hiyo, hofu nyingi tulizo nazo ukubwani ni matokeo ya kile tulichojifunza kutoka kwa jamii inayotuzunguka.

Ni hofu gani uliyokuwa huna utotoni lakini sasa unayo, na unadhani uliijifunza kutoka wapi?
 
Mtoto hatoi mitetemo imuwezayo nyoka kuona hatari thus nyoka hawezi mdhuru mtoto.
Hata simba anasoma hofu yko ili akudhuru
 
Hofu ni maumbile, ila nini cha kuogopa ndio tunajifunza kulingana na mazingira.

Ila katika hofu zoote, katika jamii zetu za kitanzania kuna hii hofu ya kuogopa, maiti/mtu aliyekufa.
Wakati kiuhalisia kama kuna mtu ambaye hajiwezi kwa lolote ni maiti, lakini ajabu watu ndio wanamuogopa kupita maelezo.

Na hii ni kutokana na yale tuyaonayo bongo movie pamoja na stori za kutishana ambazo huwa tunasimuliana.

Ila hofu hii haina uhalisia.
 
kwahiyo nyoka anatafunaga watu walio na hofu eti...🤣
Yes baada ya kustukta thus nyoka wapo wengi porini but hawavamii watu hovyo kama haujawaona hata chui unaweza mpita katulia tu mtini kama haujamuona hana time nawe
 
Yes baada ya kustukta thus nyoka wapo wengi porini but hawavamii watu hovyo kama haujawaona hata chui unaweza mpita katulia tu mtini kama haujamuona hana time nawe
Hata chui wa dar hawapo hivyo!
 
American Psychological Association
 

Attachments

  • FullSizeRender.MOV
    33.5 MB
Back
Top Bottom