Replica
JF-Expert Member
- Aug 28, 2017
- 1,681
- 8,887
Wanawake zaidi wanajifungulia nyumbani kutokana na hofu ya Covid 19 huku vifo vikiwa haviripotiwi kwa mamlaka husika, takwimu zilizotolewa na serikali zimesema.
Kwenye ripoti ya CRS imesema idadi ya vizazi iliyosajiliwa imeshuka kwa asilimia 13.3 na usajili wa vifo ukipungua kwa asilimia 15 tangu nchi ya Kenya ilipopata mgonjwa wa kwanza wa corona Machi 13.
Wanawake wajawazito wanahofia kuambukizwa corona mahospitalini na wengine kushindwa kuzifikia huduma za afya kutokana na vizuizi vya mizunguko hivyo wengine kuamua kujifungulia nyumbani.
CRS imesema takriban vizazi 40,000 inawezekana havijasajiliwa mwezi May ambapo vizazi 71,502 pekee ndio vimesajiliwa ikilinganishwa na 110,792 vilivyosajiliwa mwezi Mei mwaka jana ikiwa ni anguko la asilimia 35.3.
Mimba za utotoni zimeendelea kushika kasi ilhali vifo vinavosajiliwa vinaendelea kupungua na inahusishwa na sheria ya covid19 ambapo wahanga wanatakiwa kuzikwa ndani ya saa 24 hivyo wengi kutochunguzwa sababu ya kifo(Post mortem).
Mkurugenzi wa afya nchini Kenya, Patrick Amoth amesema siku zijazo kutakuwa na watoto wengi ambao hawajapata chanjo hivyo ugonjwa wa mlipuko ukitokea mathalan kipindupindu uwezekano wa wao kuishi ni mdogo na kuwahakikishia wakenya usalama wa vituo vya afya kwani kujifungulia nyumbani na kumnyima mtoto chanjo na kinga muhimu itasababisha janga kubwa siku zijazo.