Pre GE2025 Hofu ya Uchawi na Ushirikiana yatanda miongoni mwa Wagombea Uongozi na Wajumbe wa Mkutano Mkuu wa CHADEMA kuelekea Uchaguzi wa ngazi ya Taifa

Pre GE2025 Hofu ya Uchawi na Ushirikiana yatanda miongoni mwa Wagombea Uongozi na Wajumbe wa Mkutano Mkuu wa CHADEMA kuelekea Uchaguzi wa ngazi ya Taifa

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)

Tlaatlaah

JF-Expert Member
Joined
May 18, 2023
Posts
24,665
Reaction score
25,388
Tayari wagombea uongozi wa nafasi mbalimbali za chadema taifa na wajumbe wa mkutano mkuu wameanza kushikana, uchawi, kulaumiana na kutuhumiana kufanyiana ushirikiana kuelekea katika chaguzi za BAVICHA, BAWACHA, BAZECHA na ule uchuguzi wa kamati tendaji ya chadema taifa utakaonza mapema mwezi huu wa Jan.2025

Kushika kasi kwa matumizi ya ushirikiana na uchawi kutafuta uongozi miongoni mwa wanachadema wanaogombea, kumezua hofu na taharuki za kiusalama kwa jamii mbalimbali nchini.

Wagombea na wajumbe wapigana vikumbo kwa wanganga wa kienyeji kusafisha nyota na kutafuta ushindi.

Chonde Chonde Chadema msithubutu kuumiza familia za watu kwa imani za kichawi kwasababu tu ya tamaa binafsi za kutaka kua viongozi hali ya kua hamna uwezo, hoja wala sera nzuri. Lakini pia msiliabishe Taifa letu kwa ushirikiana eti katika kutafuta uongozi.

Tumieni sera, mipango mikakati bora ya kisiasa katika kushawishi wapiga kura wenu na hatimae kushinda uchaguzi. Chuki, mihemko, uzushi na ushirikiana ni fedhaha sana kwa wanasiasa wasomi.

Ndugu mdau wa siasa JF, unaamimi uchawi na ushirikina katika kupata uongozi?🐒

Mungu Ibariki Tanzania,
Mungu epusha athari za ushirikiana na uchawi kwa waTanzania wasio na hatia.
 
Back
Top Bottom