Rutashubanyuma
JF-Expert Member
- Sep 24, 2010
- 219,468
- 911,184
Walimu wagoma kurejea kazini
na Moses Ng'wat, Mbeya
WANAFUNZI wa shule ya msingi Chindi, wilayani hapa wameshindwa kuanza masomo kutokana na walimu wao 12 kugoma kuendelea na kazi shuleni hapo licha ya kuhakikishiwa usalama.
Mwishoni mwa mwaka jana, walimu 12 wa shule hiyo iliyoko Kata ya Msangano, walikimbia shule hiyo kwa madai ya kufanyiwa ushirikina. Hata hivyo serikali ya wilaya kwa kushirikiana na viongozi wa kimila waliingilia kati sakata hilo na kutangaza kulimaliza huku wakiwaomba walimu hao kurejea kazini.
Baadhi ya walimu hao walipohojiwa na Tanzania Daima, walisema hawako tayari kurudi kufanya kazi katika mazingira ya shule hiyo kwa kuwa yanahatarisha usalama wao licha ya serikali kutoa agizo la kuwataka warudi.
Katika mahojiano hayo, walimu hao walisema msimamo wao ni kumtaka mkurugenzi wa halmashauri hiyo kuwapangia vituo vingine vya kazi badala ya kuwalazimisha kuendelea kufanya kazi katika mazingira ambayo tayari yamewaathiri kisaikolojia.
Hata hivyo, walieleza kuwa endapo uongozi wa wilaya hiyo hautasikiliza hoja yao ya kutafutiwa vituo wapo radhi kuacha kazi.
Mratibu elimu kata wa Msangano, Osia Mwanyamba, alithibitisha shule hiyo kushindwa kuanza kazi kutokana na kukosa walimu baada ya walimu wote 12 waliokuwa wakifundisha kugoma kurejea shuleni hapo.
Mkuu wa wilaya ya Mbozi, Gabriel Kimolo, alipohojiwa kuhusiana na suala hilo alisema hajapata taarifa ya walimu hao kutoripoti katika kituo chao cha kazi na kuahidi kulifuatilia.
Desemba mwaka jana, walimu walianza kuanguka na kupoteza fahamu, wengine kuona giza wanapokuwa wakifundisha darasani, na wakati mwingine kujikuta wamelala nje ilihali walilala ndani vitendo ambayo viliripotiwa kuwa ni vya kishirikina.