JEKI
JF-Expert Member
- Aug 16, 2013
- 4,845
- 2,957
Rais amekuwa akisisitiza sana kama katiba mpya haitapatikana basi ya zamani itaendelea, tunajua wapo watu wengi ndani ya utawala hawataki katiba mpya wanaweza kutuletea kitu cha hovyo ili tukikatae wao wapete. Nimejiuliza sana hivi suruhu ya katiba mpya ikikataliwa ni kuendelea na ya zamani tu? hakuna njia nyingine? kwa kweli iwavyo tusikubali kurudi kwenye katiba ya zamani, mfano kikatokea kipengere kimoja tu kibovu, je tuikatae yote?.
Tiba ya hoja hapo juu ni hii, kwa kuwa wengi hatutaki katiba ya zamani, basi siku ya kupiga kura tupigie kura rasimu hii iliyotolewa na Warioba na ile itakayotolewa na bunge la katiba, pia napendekeza vipengele vyote tata tuvipigie kura separate, mfano suala la muungano kuwe na kipengele cha wanaotaka serikali 1, 2 au 3 na itakayoshinda ndo iingizwe kwenye katiba mpya, hii ni kuzuia kipengele kimoja au viwili kukwamisha katiba nzima.
Karibuni tuchambue.