Hofu yatanda jangwani. Hawajui wafanye nini, waanza kuzua malalamiko

Cashman

JF-Expert Member
Joined
Jun 8, 2018
Posts
3,017
Reaction score
5,294
Ni picha la kutisha sana muuaji wa jangwani yupo tena kwa ajili ya kazi hiyo.

Hofu kubwa imetanda katika mioyo ya wana jangwani kwa kuwa hawajui hatma yao kwa sasa na wameanza kutumia njia yao maarufu ya kutafuta huruma.

Njia hii ya malalamiko ilifanya waonewe huruma na baadhi ya watu walioamua kujiunga nao.

Mwaka huu ni wa malalamiko sana kwa TFF,serikali,waamuzi,CAF na hata waandishi wa habari wa kimataifa wanaomposti mpinzani.

Poleni sana "utopolo msiyempenda kaja"
 
Timu yetu imeweka kambi uturuki wiki 3 na mwekezaji anasema ameweka bilioni tatu za usajili, lakini bado uwanjani tulihitaji refa abebe aibu yetu!!!
Itakuwaje sasa tunaenda kutana na Bingwa mtetezi?

Sent from my SM-A032F using JamiiForums mobile app
Msiyempenda kaja! Jumapili mtatukana matusi yote kwa TFF mtapigwa mpaka Mchakae.
 
Simba imebebwa.

TUKIWAAMBIA Simba ni timu mbovu mno.

Pale Katikati pana shida mno.

Tuliwaaambia Inonga au malone AKIUMIA ni mtihani.
Leo Inonga AMEUMIA.

1. Hakuna Golikipa wa maana.

2. Hakuna namba 5 wa kuwachallange Inonga na Malone.

3. Hakuna kiungo mkabaji No 6

4. Bado No 9.
Baleke anaonekana Ana presure anapania sana, Jukwaa linamtesa sana.

TATIZO WAMEJAZA MAWINGA.
 
UAJIULIZA ANAYEFANYA USAJILI WA MAWINGA ANAAKILI TIMAMU KWELI?????????
.
Mawinga. 2023
1. Peter Banda.
2. Jimyson Mwinuke.
3. KIBU Denis.
4.Said Ntibazonkiza.
5. CLOTUS Chama 10-11.
6. Aubin Kramo.
7. Essomba Onana.
8. Luis Miquesson.
.
Hili KOSA lilifanyika 2020.
Mawinga walikuwa kumi, ukiunganisha idadi Yao mchango WAO MAGOLi hayafiki hata 10.
.
1 Bernald Morison.
2. Perfect CHIKWENDE.
3. Hassan Dilunga.
4. Ibrahim Ajibu.10--⁷
5.peter Banda.
6.pape sackho
7. Dunkan Nyoni
8. Valentine Muhilu.
9. KIBU Denis.
10. RALY BWALYA 8-10--11.
.
UNAJIULIZA HUU USAJILI UNAFANYWA NA MTU MWENYE AKILI TIMAMU KWELI
 
Naona unatumia reverse psychology. Hofu ya Simba umeigeuza hofu ya Yanga. Huku ni kujifariji kwa sababu unajua kitakachitokea J2.
 
Simba shida kocha akiweka music mzuri 45 Yanga hufiki, Saido ,kibu Bocco, mzamiru wasicheze hakuna wa kusimama
 
Yan hofu itande kwa Yanga dhidi ya timu inayotabirika? Akikosekana Chama mipira haitembei. Yule Malonya akikosa partner shughuli imeisha. Kwa kilichotokea dhidi ya Singida aibu naona mimi maana sio kwa mahaba yale ya refa. Mnawekwa mgongoni ila bado hambebeki
 
Kwa pira "makande" mlilocheza na singida mjiandae kwa kipigo tu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…