Red Giant
JF-Expert Member
- Mar 9, 2012
- 15,657
- 20,967
Nimeonelea nilete hii mada kwa mara ya pili.
Maelezo kwa mtumiaji ni muhimu sana hasa kwa vitu kama dawa. Sasa unakuta bidhaa inauzwa Tanzania na nyingine inatengenezwa hapahapa lakini inakuwa na maelezo ya Kiingereza, Kifaransa, kiarabu na lugha zingine lakini si Kiswahili.
Watumiaji wengi wa nchi hii wanajua Kiswahili tu, sasa maelezo ya hivyo yanamlenga nani? Kiingereza ni lugha rasmi lakini ni wangapi wanaielewa?
Watu wanatumia kitu bila kujua madhara yake na kumbe yameandikwa hapohapo ila shida lugha. Mtu unashindwa kurekebisha kaishu kadogo kumbe utatuzi umeandikwa hapohapo.
Mtu unanunua sabufa yako kali ila unashindwa kuconnect na maelezo ya kuconnect yameandikwa hapohapo.
Unanunua dawa, maelezo ya madhara na namna ya kutumia yameandikwa hapo ila unatumia upo gizani.
Mi nashauri bidhaa yeyote isisajiliwe kuuzwa Tanzania kama haina maelezo ya mtumiaji kwa lugha ya kiswahili. Iwe simu, TV, gari, dawa yaani bidhaa zote. Au nakosea ndugu zangu?