Hoja binafsi kuhusu H. pylori

Hoja binafsi kuhusu H. pylori

mamajoo

Member
Joined
Apr 19, 2012
Posts
5
Reaction score
3
Nauliza kwamba h. pylori inampataje mtu ambaye anajilinda sana kwenye chakula n.k.? Mtu anayekula kwa wakati kwa mfano usiku anakula kabla ya saa mbili, hatumii sukari (anatumia sukari mbadala mara moja moja), hali vitu vya kukaanga, hali nyama nyekundu, hatumii mafuta kwenye chakula chake cha kuchemsha n.k. Sasa huyu mtu anapataje h. pylori?
 
H-pylori huambukizwa kwa njia mbalimbali kama:

-kupitia uchafu kwenye chakula, maji na vyombo vinavyotumika kulia au kuhifadhi vyakula/vinywaji

-mdomo kwa mdomo- kuhusu, hasa kama mmoja tayari ana maambukizi ya H-pylori

-kupitia kinyesi na matapishi
 
Jinsi ya Kujikinga:

✅ Osha mikono na sabuni kabla ya kula na baada ya kutoka chooni.
✅ Kunywa maji safi na salama.
✅ Kula chakula kilichoandaliwa kwa usafi.
✅ Epuka kula chakula kilichoachwa wazi kwa muda mrefu.
✅ Tumia vyombo vya kula vya kibinafsi ikiwa kuna shaka ya maambukizi.
 
Naona Mkuu kuna kitu hapo hauna ufahamu nacho sawa sawa, iko hivi:

(A) H.Pylori ni bakteria wanaosababisha madonda ya tumbo, ambapo ukipata maambukizi ya hawa bakteria haijalishi unakula chakula kwa wakati au ni aima gani ya chakula, wenyewe watapenya kwenye kuta za tumbo lako na kusababisha nyufa katika kuta za tumbo lako ambayo ndo tunaita madonda ya tumbo.
Katika haya maambukizi ya bakteria hawa ukienda hospital utaandikiwa kipimo cha H.Pylori ili kuhakiki kama madonda yako ya tumbo yamesababishwa na bakteria hawa. Kipimo chake ni kwa njia ya Damu au haja kubwa (Stool antigen test).

(B) kuna madonda ya tumbo (Peptic ulcers) yanayosababishwa na Kemikali za tumbo (Hcl acid) zinaunguza kuta za tumbo na hii sasa husababishwa kwa asilimia kubwa kutokaka na kutokula chakula kwa wakati au kishinda njaa mara kwa mara.
Hapa utapimwa hospital kwa njia ya kuingiziwa kifaa kwa njia ya mdomo mpaka tumboni ambacho kimefungwa camera ndogo na kitaonesha tumbo lako kwa ndani kupitia Screen, njia hii tunaiita ENDOSCOPY.
 
Mzee h.pylori unapata hata kwa kula denda tu, unakula ndenda na mwanamke/mwanaume mwenue vimelea vya pylori kesho kutwa tu unanasa kwenye mtego.
 
Back
Top Bottom