Hoja Fukunyuku: Che Malone ahamishwe awe kiungo mshambuliaji

SAYVILLE

JF-Expert Member
Joined
Mar 25, 2010
Posts
7,895
Reaction score
12,975
Kama umemfuatilia Che Malone ni beki aliye na uwezo wa kupiga chenga, ana nguvu, ana composure nzuri akiwa na mpira, ana uwezo wa kufunga na kukimbia na mpira. Haya yote anayafanya akiwa anacheza nafasi ya beki wa kati. Imagine akiwa anacheza mbele kidogo.

Siku moja kocha Fadlu ajitoe ufahamu, beki za kati pale amuweke Hamza na Chamou au Kazi, namba 10 amuweke Che Malone uone jinsi mbele pale patakavyofunguka na nafasi nyingi za magoli kutengenezwa.

Inawezekana dirisha dogo kupata beki wa kati ni rahisi zaidi ya kupata kiungo mshambuliaji na hii inaweza kuwa suluhisho la tatizo. Simba bado inajenga timu kwa hiyo isiogope kufanya majaribio kama haya, hauwezi jua yatakupa nini.
 
Wampeleke akavue perege huko Ifakara.
 
Yupo slow sana, kuna siku alicheza namba sita ni kituko cha karne, acheze pale pale anapocheza ndo anafit 100%
Speed yake haitofautiani sana na ile ya Ahoua na naona kama Che Malone anakupa vitu vya ziada zaidi.

Kama angekuwa slow kama unavyosema usingeshauri aendelee kucheza nafasi nyeti kama beki wa kati. Anacheza kwa timing na composure nadhani hilo ndiyo linafanya wengi tunatafsiri kama yuko slow.
 
No 10 hapana, ila 6 anaweza kabisa....lakini wana Okajefa apewe muda anafiti vizuri tu.
 
aliwahi kuchezeshwa dimba la kati ila alizingua mj naona aendelee kucheza centerhalf.
 
Back
Top Bottom