Hoja: Jina sahihi la Kiswahili ni Russia au Urusi?

Kibosho1

JF-Expert Member
Joined
Dec 12, 2017
Posts
2,621
Reaction score
4,293
Kutokana na mgogoro uliopo hapo ulaya nimesikia kwenye vyombo vya habari mbalimbali lakini vikitaja majina tofauti.

VOA, Mwananchi,Milard Ayo wanasema,wanatamka au kuandika jina Russia lakini BBC,DW wanaripoti jina Urusi.

Sasa swali ni jina gani la kiswahili sahihi kutumika? Russia ni kingereza au kiswahili na je Urusi ni nini?

Karibuni
 
Urusi ni Kiswahili Russia English.
Kwenye Kiswahili uwa tunaongeza U kwenye majina ya nchi nyingi mfano England-uingereza, Germany- Ujerumani, Phillipines - Ufilipino
 
Hawa wanaotaka Russia wanapata wapi ujasiri
 
Umbeya..
Hii formula ni kwa bara la ulaya tu..amerika,africa na asia hawamo nadhani
 
Tungelikuwa tumeanza kuita hayo majina na kuyazoea tokea zamani basi leo tungeona kawaida tu.

Mfano neno "Uchina" kama halinpgi hivi kutamka hivyo ila kadri siku zinaavyoenda litazoeleka tu.
 
U- inatumika zaidi katika nchi ambazo katika wakati husika au nyakati fulani ziliwahi kuwa milki (Empire).

Urusi iliwahi empire.

Mfano:

United Kingdom - Uingereza
Great Britain - Britania.

Persia - Uajemi.
Irani - Iran.

Nadhani nimeeleweka.
...
 
Kutokana na mgogoro uliopo hapo ulaya nimesikia kwenye vyombo vya habari mbalimbali lakini vikitaja majina tofauti.

VOA, Mwananchi,Milard Ayo wanasema,wanatamka au kuandika jina Russia lakini BBC,DW wanaripoti jina Urusi.

Sasa swali ni jina gani la kiswahili sahihi kutumika? Russia ni kingereza au kiswahili na je Urusi ni nini?

Karibuni
FANYENI KAZI NYIE
 
Back
Top Bottom